TAARIFA YA HABARI KUTOKA RADIO SENGEREMA FM
KUMALIZA
ZIARA.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Kongo Joseph Kabila amemaliza
ziara yake ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini na kurejea nchini
kwake.
Akiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl ,Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam Rais Kabila ameagwa na mwenyeji wake Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli.
Katika hatua nyingine, mara
baada ya kuondoka kwa Rais Kabila,
Rais Magufuli amefanya ukaguzi wa kushitukiza katika
sehemu ya kukagulia mizigo na abiria ya uwanja huo upande wa Terminal One ambapo Mwezi Mei mwaka huu
alitembelea kwa kushitukiza na kubaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners) zilikuwa hazifanyi kazi.
Mara hii Rais Magufuli amebaini kuwa mashine hizo
zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye mwenyewe uhalisia wa namna mizigo
inavyokaguliwa.
Hata hivyo amemuagiza
Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha kuwachukulia
hatua za kinidhamu maafisa wawili walitoa taarifa za uongo pindi alipofanya
ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.
Na,
Mhariri Twimanye Chanzo Millad ayo
MAJI
Wananchi wa katika
kitongoji cha KABAGANGA kisiwani KOME katika halmashauri ya
Buchosa mkoani MWANZA
wameiomba serikali kuwachimbia visima ili kukabiriana na tatizo lililopo la maji.
Wakielezea hali hiyo wananchi hao wamesema kuwa huwalazimu kuamka majira ya saa nane za usiku na kurudi
nyumbani saa nne za asubuhi hari inayopelekea kukwamisha shughuli za kila siku
za maendeleo.
Hata hivyo kwaupande wake mwenyekiti wa kitongoji hicho cha KABAGANGA KATI Bwana SAMWEL
JOHN amekiri kuwepo kwa hali hiyo.
Na, Marlesa/ Mhariri Twimanye Chanzo Mahojiano.
CHAMA CHA WALIMU
Chama cha Walimu Mkoa wa Mwanza kimeituhumu ofisi ya mkurugenzi wa
Jiji la Mwanza kuhusika na kugushi takwimu za
idadi ya wanafunzi na
kusababisha kuwepo wanafunzi hewa 5559 .
Akisoma tamko la walimu hao katibu wa chama cha Walimu
Wilaya ya Nyamagana Asha Juma amemtaka mkurugenzi wa jiji kuwaomba radhi walimu wakuu 62,
waliosimamaishwa kazi kwa tuhuma zakuandaa orodha za wanafunzi hewa katika
shule zao vinginevyo kitamfikisha mahakamani.
Baadhi ya walimu waliofukuzwa kazi wamezishangaa takwimu zilizotumika
kuwasimamisha kazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Kihomoni Kibamba amesema hayuko tayari kuwaomba radhi
walimu hao na kwamba endapo hawajaridhika na hatua aliyoichukua wapeleke mamalamiko ya katika tume
ya utumishi wa walimu.
Chama cha Walimu Wilaya ya Nyamagana kimetishia
kwenda mahakamani endapo mkurugenzi wa jiji hilo hatawaomba radhi walimu hao waliosimamishwa
kazi na kutengua barua aliyowaandikia.
Na, Mhariri
Twimanye Chanzo TBC.
BARABARA.
Wakazi wa Kijiji cha Balatogwa kilichopo kata ya Mwabaluhi Wilayani Sengerema
,wamelalamikia kitendo cha baadhi ya viongozi waliotoa ahadi
ya kukarabati barabara
itokayo Mjini Sengerema
hadi Ngoma kwa kushindwa kutekeleza ahadi hiyo kwa wakati.
Katika mahojiano na Radio Sengerema wananchi hao
wamesema licha ya viongozi hao kutoa ahadi ya kutengeneza barabara
hiyo kabla ya msimu wa masika
kuanza wataikarabati lakini mpaka sasa bado ni kitendawili.
Wamesema kuwa
kwa sasa wamekuwa na mashaka na viongozi hao juu ya kukamilisha ahadi
hizo kwani kiongozi bora
hujali matakwa ya wananchi wake kwa
hutimiza ahadi mapaema.
Kufuatia malalamiko hayo ya wananchi Radio Sengerema
imemtafuta mewenyekiti wa kijiji cha Balatogwa Bwn,Joseph Nzungu John ili
kujibu malalamiko hayo ya wananchi ambapo amesema serikali ya kijiji hicho
inatarajia kuitisha kikao ili kuitafutia ufumbuzi kero hiyo.
Ubovu wa barabara itokayo Mjini Sengerema hadi Ngoma
imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu sasa bila kupatiwa ufumbuzi
wowote.
Na,
Mhariri Twimanye Chanzo
Mahojiano.
KUSIMAMISHWA
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Mrisho Mashaka Gambo, amewasimamisha
kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za uchaguzi wa mwaka
2015.
Watumishi waliosimamishwa
kazi ni pamoja na Bi. Hadija Mkumbwa ambae
alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa mwaka jana na kumfuta cheo hicho, Bwana Evansi Mwalukasa aliyekuwa mwekahazina wa halmashauri na
bwana Sembeli Sinayo aliyekuwa mwanasheria wa halmashauri.
Maamuzi hayo yamefikia
baada yakubainika kuna upotevu wa fedha za uchaguzi takribani Milioni 188
ambazo matumizi yake hayakuwekwa wazi na pia Milioni 20 zilitumika kwa manunuzi
ambayo hayakufuata taratibu za manunuzi ya serikali.
Aidha Muheshimiwa Gambo alisema maamuzi hayo yametokana
na taarifa aliyokabidhiwa na kamati aliyoiunda yakuchunguza mapato na matumizi
ya fedha za halmashauri hiyo na kubaini upotevu huo wa fedha nyingi ambazo
zingeweza kusaidia shughuli mbalimbali za uchaguzi katika Wilaya hiyo.
Na, Mhariri
Twamanye Chanzo Dewji.
KIMATAIFA.
Mwanamme huyo wa miaka 43 hajawahi kuonekana
hadharani tangu kuacha shule akiwa na miaka 13.
Aidha Polisi wamesema japo mwanamme huyo yuko
shwari kiafya, hata hivyo ameonekana kuwa na mfadhaiko.
Na, Mhariri Twimanye
Chanzo BBC.
KIMATAIFA.
Mageuzi makubwa yanahusu
wizara ndogo mpya iliyoundwa katika wizara ya sheria ikihusu maswala ya katiba
na sheria nyingine.
Wizara hiyo ndogo
imepewa Bwana Evode Uwizeyimana ambaye wengi nchini Rwanda
walimfahamu kama mkereketwa wa upinzani dhidi ya utawala wa RPF kabla ya
kurejea nchini miaka 2 iliyopita akitoka uhamishoni nchini Canada.
Mara baada ya kurejea
nchini Bwana Uwizeyimana alijumuishwa katika tume ya Rwanda iliyofanya
mabadiliko ya katiba ambapo rais Kagame aliongezewa muda wa kukaa madarakani.
Rais Kagame amembadilishia wizara Dr Diane
Gashumba aliyekuwa waziri wa familia na usawa wa jinsia na kumweka katika
wizara ya Afya,wadhifa uliokuwa wazi tangu kufutwa kazi kwa Dr Agnès Binagwaho
miezi mitatu iliyopita.
Aidha wizara ya maswala
ya nchi za Afrika Mashariki imeunganishwa na wizara ya biashara inayoendelea
kuongozwa na François Kanimba.
Aliyekuwa waziri wa maswala ya jumuiya ya Afrika Mashariki Bi
Valentine Rugwabiza ameteuliwa kuwa balozi wa Rwanda katika Umoja wa mataifa.
TAMATI YA TAARIFA YA HABARI
Post a Comment