TAARIFA YA HABARI KUTOKA RADIO SENGEREMA FM
KIFO.
Mwalimu wa shule ya
Msingi Kizugwangoma Kata
ya Mission Wilayani Sengerema Mkoa mwanza George Mtaki amekutwa
amefariki na mwili wake ukiwa babarabani majira ya saa 12.20 asubuhi.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Igogo Kata ya Nyampulukano Goodluck
Daudi amesema alipigiwa simu majira ya saa 12:20 asubuhi kuwa katika eneo
lake karibu na kanisa la Babtisti
barabara iendayo Hosipitali teule ya Wilaya kuna mtu amefariki
dunia.
Bw, Daud amesema kuwa hapo awali
mwalimu huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa pumu mazingira waliyomkuta
akiwa amepoteza maisha inaonekana wazi kuwa alikuwa akielekea hospitali kupata matibabu kwa kuwa walimkuta
ameshikilia fedha na dawa aliyokuwa akitumia.
Mgaga mkuu wa Hosipitali teule ya Sengerema
Sister Mary Jose
amethibitisha kupokea mwili huo na baada ya kuuchunguza walikuta hana jeraha
lolote katika mwili wake na walikuta maji ndani ya tumbo na inawezekana kwa
kuwa alikuwa na ugonjwa wa pumu inaonekana wazi kuwa ndiyo umepelekea kifo
chake.
Jeshi la Polisi Wilayani
Sengerema limethitisha kutokea kwa kifo hicho.
BARABARA
Abiria
wanaotumia barabara itokayo sengerema kuelekea Ngoma wameilalamikia barabara
hiyo kutokana na ubovu hali inayosababisha usumbufu mkubwa wakati wa kusafiri.
Barabara
hiyo wameeleza ni kiungo kikubwa katika usafirishaji wa bidhaa mbalimbali hivyo
ubovu huo unakwamisha shughuli za maendeleo kwa wakazi wa maeneo hayo.
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya Igalula
Mhe,Onesmo Mussa Mashili amesema
barabara hiyo ilisuasua kutokana na
ukosefu wa fedha ambapo kwa sasa tayari pesa imekwishapatikana na mkandarasi
novemba mwaka huu ataanza ukarabati mara moja ili kuwaondolea adha wakazi wa
kata hiyo.
Hata
hivyo diwani huyo amemshukuru mkuu wa wilaya ya sengerema bw Emmanuel Kipole baada ya kuingilia kati kutokana na mkandarasi kushindwa kuanza kazi kwa wakati ambapo
alipaswa kuanza kazi tangu Octoba 6,mwaka huu
hivyo amemuaru kuanza kazi hiyo mara moja.
Na Veronicah/Paulina Chanzo;Mahojiano.
WAZEE
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema
Emmanuel Kipole amezita
mamlaka husika ziache tabia ya
kuwatoza fedha za matibabu wazee wanapofika
hospitalini kupata matibabu.
Kauli hiyo ameitoa Katika Kata ya
Kafunzo Halimashauri ya Buchosa Wilayani humo baada ya Kikundi cha
wazee cha kata hiyo kiitwacho UWAKA kumlalamikiamkuu huyo wa wilaya
kutozwa fedha wanapofika kupata huduma za afya kinyume na sera ya wazee.
Amesema kuwa Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Taifa imepitisha sheria ya wazee
kuanzia miaka 60 kupata huduma bure za matibabu katika Zahanati na
hosipitali zote nchini kwa kuzingatia kuwa kundi hilo halina uwezo wa
kujihudumia katika swala la fedha za matibabu.
Kipole amesema kuwa zama za kuwatoza wazee zimekwisha hivyo huduma hiyo inapaswa
kutolewa bure na mtumishi yoyote wa afya atakaye watoza fedha
za matibabu wazee waliofika kupata matibabu au kuwanyanyasa wazee wakati wakipata matibau hata vumiliwa na
atakuwa amejifukuzisha kazi .
Na,Paulina
Chanzo:Mahojiano.
MAZINGIRA.
Halimashauri ya
Wilaya Sengerema imeagizwa
kuunda vikundi vya usafi wa mazingira kila kata kwa lengo la kuondokana na adha
ya uchafu unaotokana na kuzalishwa na wananchi wa maeneo mabailimabali katika
mji wa Sengerema.
Kauli hiyo imetolewa
na Mkuu wa Wilaya Sengerema Emmanuel
Kipole alipokutanana na wenyeviti wa mitaa
na Madiwani wanaounda mamlaka
ya mji mdogo wa Sengerema katika
kikao cha pamoja kwa lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwemo swala la usafi
wa mazinga na ulinzi na usalama.
Amesema suala la
usafi wa mazingira ni jukumu la kila raia
hivyo wanapaswa kuwajibika katika swala hilo ili mji na mazingira yawe safi kwani kwa kufanya hivyo watatumisha afya na kuepukana na kukumbwa na magonjwa ya
mlipuko hasa kipindupindu.
Na,
Said/Paulina
Chanzo:Kikao
KIMATAIFA
Mdahalo wa pili wa wagombea
urais wa Marekani Hillary Clinton na Danald Trump umefanyika leo hii.
Kampeni kwa upande wa chama
cha Republican ipo katika mtikisiko
baada ya kuvuja kwa mkanda wa video wa mwaka 2005 uliyomrekodi Trump akizungumza maneno machafu dhidi
ya wanawake.
Ikiwa uchaguzi wa Marekani unatarajiwa kufanyika si zaidi
ya mwezi mmoja, idadi kadhaa ya wabunge waandamizi wa chama cha Republican wamejiondoa katika kumuunga
mkono bilionea huyo.
Trump mwenyewe amesalia kuwa
mkaidi pamoja na miito ya kumtaka ajiondoe katika kinyang'anyiro hicho.
Kabla kuanza mdahalo huo
katika ukumbi wa Chuo Kikuu Washington,
St. Lous viongozi hao wawili walishindwa kupeana mikono.
Na,
Paulina Chanzo:DW.
KIMATAIFA
Serikali ya Ethiopia imetangaza miezi sita ya hali
ya hatari nchini kote kufuatia kufanyika maandamano ya wanaoipinga serikali
ambayo yamesababisha watu kadhaa kupoteza maisha.
Akizungumza kupitia
televisheni, Waziri Mkuu Hailemariam
Desalegn amesema machafuko hayo yameathiri mali na kutishia utulivu wa
taifa na usalama.
Miji mikubwa na midogo
katika eneo la Oromia nchini Ethiopia kumeshuhudiwa vurugu za
maandamano ya watu wanaodai uhuru zaidi.
Zaidi ya watu 50, walikufa
katika mkanyagamno ulitokea juma lililopita, baada ya polisi kuwafyatulia
mabomu ya machozi na risasi kuwawatawanya waandamanaji hao wanaoipinga
serikali.
Maandamano yalianza mwaka
uliopita kutokana na hofu kwamba mpango wa serikali kuongeza mpaka wa Addis Ababa ungewapokonya baadhi ya
wakulima maeneo yao.
MWISHO
WA TAARIFA YA HABARI
Post a Comment