TAARIFA
YA HABARI KUTOKA RADIO SENGEREMA FM
TUKUIO.
Jeshi la polisi
mkoani Pwani ,limewakamata watoto
22 wa madrasa ya Arahma pamoja na
mwalimu wa madrasa hiyo ambae alikuwa akiendesha mafunzo ya kigaidi kwa watoto
hao, Kimarang’ombe ,kata ya Nianjema
Bagamoyo.
Kwa
undani wa habari hii , usikose kufuatilia taarifa hii katika uchambuzi wetu wa habari kwa kina muda
mfupi ujao.
HAKI ELIMU.
Shirika la haki Elimu
na Kituo cha
Sheria na haki za Binadamu, wamelaani kitendo cha adhabu
ya kikatili aliyopewa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Mbeya Sebastian Chinguku na walimu wa shule
hiyo.
Akiongea na waandishi wa habari, leo Mkurugenzi Mtendaji wa Haki Elimu, John Kalage, amesema vitendo kama hivyo
vinachangia kwa kiasi kikubwa watoto wengi hususani wa kike kuacha shule, hivyo
kukosa haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Pia ameishauri serikali juu ya uboreshaji wa utoaji wa taarifa
dhidi ya matukio ya kikatili kama hayo yanapotokea.
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa,serikali inatakiwa kuboresha
miongozo yake ya kusimamia na kuimarisha nidhamu shuleni na kuhakikisha
inazingatiwa na watu wote.
Kwa upande wake Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu,
kimepongeza mshikamano uliooneshwa na wananchi katika kukemea ukatili huo.
Na, Mhariri
Twimanye chanzo Mpekuzi
UKOSEFU WA MADARASA
Wanafunzi wa darasa la
kwanza hadi la tatu wa Shule ya msingi Chikomelo iliyopo kijiji cha Ngoma wilaya ya Sengerema wamelazimika
kusomea darasa moja kutokana
shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa madarasa.
Mwanahabari wetu SAID
MAHELA ametembelea katika shule hiyo na
kutuandalia taarifa ifuatayo.
Hayo yamebainika wakati
Diwan wa kata ya Ngoma Mh.Onesmo Mussa
Mashili alipokuwa akiongea na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika
kitongoji hicho.
Mh.
Onesmo amekiri
kuwepo kwa tatizo hilo na kuwaomba wananchi kushirikiana kwa pamoja kujenga vyumba vya madarasa.
Aidha diwani huyo amewaomba wananchi wa kitongoji hicho
wahakikishe wanaweka utaratibu mzuri wa kuchangia michango kwa ajiri ya
maendeleo ya kitongoji chao.
Na,Said
/Mhariri Twimanye Chanzo
Mkutano.
WAZEE
Kufuatia tamko la
serikali kuwa wazee wote hapa nchini wanatakiwa
kupatiwa matibabu bure, baadhi ya wazee Wilayani Sengerema ,wamepongeza
huduma zinazotolewa katika hospital
teule ya wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.
Wakizungumza na Radio
Sengerema, wazee hao wamesema kwa sasa wamekwisha pewa vitambulisho vya
kuwatambulisha ili wakati wowote
watakapohitaji matibabu waweze kupata kwa urahisi tofauti na hapo awali hawakuwa na vitambulisho hivyo.
Wameeleza kuwa hapo awali walikuwa hawapati matibabu bure ,kutokana
na kukosa vitambulisho, jambo ambalo
limekuwa likisababisha usumbufu mkubwa pindi wanapougua ikiwemo
kutopatiwa huduma ya matibabu kwani
hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Hata hivyo wameipongeza serikali kwa kutambua uwepo wa wazee hapa nchini
na kuwaomba watumishi wa sekta ya
afya waendelee kuwapa kipaumbele kwa kuwahudumia
bure bila kujali itikadi za vyama vya
siasa,dini wala kabila.
Na
,Mhoja /Mhariri Chanzo Mahojiano.
KILELE CHA MWENGE
Rais Dkt,John Pombe
Magufuli anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa
zitakayozofanyika Bariadi mkoani Simiyu, huku zikitanguliwa na maonyesho ya
wiki ya vijana.
Mbali na Rais Magufuli
katika kilele hicho, Mke wa Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere, Mama
Maria Nyerere anatarajia kuhudhuria misa ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka
17 ya kifo cha mwasisi huyo wa Taifa zitakayofanyika katika Kanisa
la Mtakatifu Yohana mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Antony Mtaka amesema
maadhimisho ya wiki ya vijana yatafunguliwa rasmi Oktoba 8 hadi 14, mwaka huu
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
wenye Ulemavu, Jenisita Mhagama
katika uwanja wa Sabasaba mjini humo
Pamoja na hayo Mtaka amesema maadhimisho hayo yataenda
sambamba na kongamano la vijana.ambapo
katika kongamono hilo kutajadiliwa mada mbalimbali zinazoihusu jamii,
ikiwemo kupinga mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
Na Veronica/Mhariri Twimanye Chanzo Mtembezi.
KIMATAIFA
Idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na kimbunga Matthew imezidi kuongezeka na
kufikia watu 478, wakati taarifa zikiingia kutoka
maeneo ya ndani ambayo hapo awali yalikuwa yamekatika kutokana na dhoruba
kali.
Wakati idadi hiyo ikiongezeka, mashirika ya serikali na
kamati tofauti zimekuwa zikitofautiana juu ya idadi kamili ya watu.
Ripoti iliyoripotiwa na shirika la habari la Reuters na kutolewa na maafisa wa asasi
za kiraia katika ngazi ya mitaa imethibitisha idadi ya vifo 478 huku
Shirika la ulinzi wa raia la Haiti
limesema watu 271 wamefariki kutokana na dhoruba na wengine 61,500 wakibakia katika mkazi.
Kimbunga Matthew pia
kimeipiga Florida katika upepo wa
kilometa 205 kwa saa na kuhatarisha
uharibifu zaidi wa miundombinu.
Na,
Mhariri Twimanye Chanzo Dw.
KIMATAIFA
Rais wa Colombia Juan
Manuel Santos ameshinda tuzo ya amani ya Nobel kwa mwaka huu, licha
ya wapiga kura kukataa mkataba wa kihistoria wa amani baina ya serikali yake na
waasi wa FARC uliofikiwa mwezi
uliopita wa kumaliza miaka 52 ya vita.
Santos ameahidi kufufua mpango wa amani licha ya kukataliwa na
raia.
Mwenyekiti wa kamati ya tuzo hiyo Kaci Kullmann wakati
akimtangaza mshindi Santos wa
tuzo hiyo, tuzo hii pia ni heshima kwa watu wote wa Colombia ambao licha yamatatizo makubwa
na ukiukwaji, hawajapoteza matumaini ya kupata amani.
Tuzo hiyo yenye thamani ya dola za kimarekani laki tisa na
elfu 30 itawasilishwa mjini Oslo Disemba
20 mwaka huu.
Post a Comment