MAFANIKIO
YA RAIS MAGUFULI.
Baadhi ya wakazi wa
Wilaya ya Sengerema wamesema Rais Dkt,John
Pombe Magufuli amefanya mageuzi makubwa
ya kimaendeleo hasa
katika nyanja ya elimu na afya
tangu alipoingia madarakani
Novemba 5 mwaka jana.
Hayo
wameyasema katika mahojiano maalumu na Radio Sengerema yaliyoangazia
mambo aliyofanya Rais Dkt,Magufuli tangu alipoapishwa na kuanza rasmi majukumu yake ya
kuiongoza Tanzania Novemba 5 mwaka jana zikiwa zimesalia
siku chache kutimiza mwaka mmoja wa
uongozi wake.
Wameeleza kuwa pamoja
na mambo mengine Rais Magufuli amesaidia
kuokoa kiasi kikubwa cha fedha walizokuwa wakilipwa watumishi hewa ambao hawafanyi kazi yoyote ya kuliingizia
kipato taifa
na kuzielekeza katika shughuli
za kimaendeleo.
KILIMO
Wakulima wameshauri
kukagua mbegu wakati wa kununua katika
maduka ya pembejeo za kilimo ili kubaini ubora wa mbengu na kuhakiki muda wa matumizi kama umekwisha.
Akifanya mahojiano na
redio sengerema ofisini kwake afisa mazao
wilaya ya sengerema bwana BERNAD
MYATIRO ameeleza kuwa wakulima wengi hushindwa kukagua mbegu kama ina ubora
ikiwemo muda wa kumalizika kwa nguvu ya mbegu hiyo na uwepo wa nembo ya tosic
ambayo huonyesha kama mbegu hiyo imeruhusiwa kisheria na kununu mbegu ambayo haioti na kumsababishia
hasara mkulima.
Aidha bwana MYATIRO ameongeza kuwa ni vyema maafisa
ugani wa kata na vijiji kutumia muda wao mwingi kuwaelimisha wakulima namna ya
kutambua mbegu bora hususani katika kipindi hiki cha kilimo ambacho wakulima
wengi huhitaji mbegu kwa ajili ya kilimo ili kuepuka hasara kubwa ambayo
wakulima wanaweza kuepuka .
Hata hivyo Bwana MYATIRO amewataka wakulima kulima mazao
ya muda mfupi na yanayoweza kukabili ukame kulingana na hali ya hewa ilivyo
hivi na mvua kuchelewa kuanza kunyesha kama vile mtama na mihogo na mahindi
aina ya DK,situka,sidiko amabazo
zinaweza kukomaa ndani ya siku 75 mpaka skiu 110.
TCU
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), kuhakikisha programu
za masomo zinazoanzishwa na vyuo vikuu nchini zinazingatia mahitaji ya Taifa na
soko la ajira.
Majiwali
ametoa agizo hilo leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 55 ya
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Amesema hivi sasa kuna baadhi ya vyuo nchini
ambavyo vinatoa programu ambazo haziendani na mahitaji halisi ya Taifa pamoja
na soko la ajira.
Kwa upande wake MKUU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Rais mstaafu Jakaya Kikwete
amekitaka chuo kikuu hicho kilinde hadhi yake ya kuendelea kuwa kiongozi katika
utoaji wa elimu bora, ambayo itasaidia taifa kuwa na wataalamu wenye kusaidia
kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili kijamii.
MKATABA
Kampuni ya Sonalika international Tractor limited ya India imesaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya Quality Group kwa ajili ya kuunda
trekta za kilimo hapa nchini.
Mkataba huo unakadiliwa kuwa na thamani ya
takriban Sh bilioni 50 mpaka 100 na umelenga kuongeza upatatikanaji wa bidhaa
hiyo kwa urahisi sanjali na punguzo la bei ili kuwanufaisha wakulima wadogo,
wakati na wakubwa.
Ofisa Masoko wa Qualiy Group Timoth Shuma amesema Undaji wa trekta hizo unatarajiwa
kuanza mapema mwaka ujao huku zikiwa na punguzo la bei la zaidi ya asilimia 30.
KIMATAIFA
Shambulio la usiku katika mji wa Mandera nchini Kenya
limetekelezwa na wanamgambo wasio al-Shabab, kwa mujibu wa mratibu wa
usalama wa eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya Bw Mohamud Saleh.
Kundi la Al-Shabab Somalia tayari limekiri
kuhusikana shambulio hilo dhidi ya nyumba ya malazi , kama tulivyoarifu awali.
Lakini Bwana Saleh amesema kutokana na kuwa mpaka na Somalia hufungwa kuanzia
usiku hadi alfajiri , hakuna namna kwa washambuliaji kuvuka mpaka huo.
Ameongeza kuwa
uchunguzi wa awali umedhihirisha kuwa shambulio hilo la saa tisa alfajiri
lilitekelezwa na magengi ya wahalifu walio na itikadi kali waliopo katika mji
wa Mandera ambao wametumia vilipuzi
vinne kuilipia nyumba hiyo ya malazi.
Watu 12 wameuawa
baada ya watu wenye silaha kushambulia nyumba hiyo ya malazi mjini Mandera.
Msemaji wa
serikali ya Kenya Eric Kiraithe
amesema watu sita wameokolewa kutoka kwenye hoteli hiyo ya Bishaaro.
KIMATAIFA
Mratibu wa shughuli za msaada za Umoja wa Mataifa, Stephen O'Brian, amezikosoa pande zote
zinazohusika katika mzozo wa vita mjini Aleppo,
siku mbili baada ya kumalizika muda wa kusitisha mapigano.
Afisa huyo amesema serikali ya Syria na waasi wanaoipinga, walizuia watu kuondoka sehemu
zilizozingirwa na upelekaji wa mahitaji muhimu kwa watu wanaouhitaji.
O'Brian amesema kutokana na hali
hiyo wameamua kuacha mpango wa kuwapelekea msaada watu waliojeruhiwa katika mji
huo wa kaskazini mwa Syria.
Aidha, mratibu huyo wa shughuli za msaada amesema ni
jambo la kukasirisha kuona pande zinazopigana, zikiweka mbele maslahi ya
kisiasa na ya kijeshi, na kuwapuuza wagonjwa, watoto na vikongwe wanaoteseka.
Umoja wa Mataifa umeshindwa kufikisha misaada katika
sehemu ya Mashariki ya Aleppo iliyo
chini ya udhibiti wa waAsi tangu mwezi Julai.
MICHEZO NA BURUDANI
Kocha George Lwandamina amemalizana na Yanga kwa maana ya mazungumzo
lakini amerejea nchini mwao bila ya kusaini mkataba na Yanga.
Kocha huyo ameondoka nchini leo
alfajiri kurejea Lusaka Zambia kwa
ajili ya kukamilisha masuala ya kifamilia.
Lwandamina ndiye anatarajiwa kuchukua nafasi ya Kocha Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi.
Kocha huyo wa zamani wa Zesco, alitua nchini juzi na kufanya
mazungumzo na uongozi wa Yanga.
======= =======
=======
Mshambuliaji nyota wa FC Barcelona, Luis Suarez ameteuliwa
kuwa mwanasoka bora wa dunia kwenye La
Liga.
Tuzo hiyo ni kwa ajili ya msimu wa
2015-16 kwa wachezaji wa La Liga.
Tuzo hiyo
hujumuisha mchezaji anayezungumzwa au aliye gumzo zaidi katika sehemu
mbalimbali duniani lakini anatokea kwenye ligi ya La
Liga.
===== ======
======
BIASHARA
Kuelekea
uchumi wa viwanda nchini, serikali imefanikiwa kufufua na kuanzisha viwanda
ambapo kwa sasa vinavyofanya kazi vipo zaidi ya 52,000. Sekta hiyo pia imetajwa
kuwa inatarajia kukuza uchumi wa watanzania asilimia 40.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage
wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonesho ya viwanda Tanzania
yanayotarajiwa kufanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam
kuanzia Disemba 7 hadi 1, 2016.
Aidha,
Mwijage amesema Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia taasisi yake
ya Mamlaka na Maendeleo ya Biashara Tanzania, imeandaa maonesho
yatakayokutanisha wadau wa sekta ya viwanda kwa lengo la kutangaza pamoja na
kujadili fursa za masoko ya ndani na nje ya nchi.
Amesema
maonesho hayo pia yatatoa taswira ya juhudi za ujenzi wa viwanda katika kipindi
cha mwaka mmoja uliopita.
Post a Comment