TAARIFA
YA HABARI KUTOKA RADIO SENGEREMA
MAKUBALIANO
Serikali za Tanzania na
Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo zimeahidi kuendeleza ushirikiano katika nyanja
mbalimbali za kiuchumi ikiwemo sekta ya uchumi ya nishati ya mafuta pamoja na
biashara.
Akizungumza na
waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli mara baada ya uwekaji sahihi mikataba ya makubaliano ya
utafutaji na uendelezaji wa mafuta katika ukanda wa magharibi mwa Afrika
mashariki katika ziwa Tanganyika.
Rais Magufuli amesema Tanzania ni sehemu
salama ya uwekezaji ambapo ametoa wito
kwa wafanyabiashara na serikali ya Congo
kuja nchini kuwekeza ili kukuza uchumi wa
nchi zote mbili.
Clip Rais Magufuli 1……..
Kwa upande wake rais wa
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Joseph Kabila amesema nchi yake
itaendelea kuitumia bandari ya Dar es salaam na kuendeleza ushirikiano kati
nchi yake na Tanzania.
Na
Veronica/Mhariri Twimanye Chanzo
TBC.
MWILI.
Hali ya taharuki imetanda katika eneo la Busaka Wilayani Chato Mkoani Geita baada ya kaburi la
mtu aliyezikwa miaka 31 iliyopita
kufukuliwa na ndugu wa marehemu
na kwenda kuzikwa katika kijiji cha Nyitundu Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza bila taarifa yoyote kwa baadhi
ya ndugu wa marehemu huyo.
Msikilizaji
usikose kusikiliza taarifa hii muda mfupi ujao katika uchambuzi wetu wa
habari kwa kina.
ONYO.
Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
imetoa onyo kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds sambamba na kukifungia
kwa miezi mitatu kipindi cha Take One
kinachorushwa na Kituo hicho.
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Method Mapunda amesema sababu ya kukifungia kipindi hicho, ni
kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na
kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha biashara ya ngono, na
kutolinda maadili ya watoto.
Aidha imeelezwa kuwa
sababau ya kufungiwa kipindi hicho ni
mahojiano kati ya mtangazaji wa kipindi hicho ambayo yalirushwa Agost 09 mwaka huu saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake.
Na, Mhariri
Twimanye Chanzo Mpekuzi.
USALAMA BARABARANI.
Kamanda mkuu wa
usalama barabarani wilayani Sengerema
mkoani mwanza Inspector Hamis Wembo amewataka waendesha pikipiki wote kuzingatia uvaaji
wa kofia ngumu wakati wa safari zao.
Amesema hayo wakati
akizungumza na Radio Sengerema ambapo
amesema nimarufuku kuendesha
pikipiki bila kuvaa kofia ngumu kwa watu wote pasipo kujali kuwa ni waendesha
bodaboda ili kujikinga na ajari.
Sanjari na hayo amesema
kuwa waendesha bodaboda wanatakiwa kuwa na kofia
mbili ikiwa moja ya dereva na nyingine ya
abiria .
Pia amesema kuwa uvaaji wa kofia ngumu ni moja ya
sheria zilizo pangwa katika kuzingatia usalama barabarani ili kuepukana na
adhabu zilizo pangwa na serikali na kwamba kwa yule atakaye vunja sheria atatozwa faini.ya shilingi elfu thelathini.
Hata hivyo amewataka waendesha pikipiki kuzingatia sheria
hiyo ya uvaaji kofia ngumu pamoja na
abiria kupenda kuvaa kofia hizo
kamakinga ya ajari.
Na arafa /Mhariri Twimanye chanzo;mahojiano.
KONGAMANO.
Makamu wa Rais Mh, Mama Samia Suluhu Hassan
amewahakikishia Wanasayansi Watafiti waliopo nchini kuwa Serikali ya Tanzania
inatambua mchango wao na wataendelea na juhudi za kuwalinda kwani ni
nguzo muhimu ya kufikia malengo ya milenia katika Nyanja mbalimbali ikiwemo
Uchumi, Afya, Elimu na Maendeleo endelevu.
Makamu wa Rais ameyasema hayo mapema leo Jijini Dar es
Salaam wakati alipozindua rasmi Kongamano la 30 la Kimataifa la Wanasayansi
Watafiti lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu
(NIMR) ambalo ni la siku tatu kuanzia Oktoba 4 hadi 6 mwaka huu.
Akiwahutubia Wanasayansi hao watafiti zaidi ya
300 kutoka Tanzania na Mataifa ya nje, amesema kuwa Taifa bila watafiti
hakuna maendeleoo hivyo uwepo wa watafiti hao ni kielelezo tosha cha kufikia
maendeleo.
Akiwaondoa hofu wanasayansi watafiti hao,
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu amebainisha kuwa, Serikali imesikitishwa na
tukio lililotokea hivi karibuni la kuchomwa moto baadhi ya watafiti huko Mkoani
Dodoma kuwa ni la kinyama na halivumiliki na sheria itachukua mkondo wake na
wahusika wote watafikishwa mikononi mwa sheria.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla katika mkutano
huo amebainisha kuwa, Wizara yake inashirikiana bega kwa bega na
wanasayansi hao.
Marekani
imesitisha mazungumzo yake na Urusi
juu ya kurejelea kwenye usitishaji mapigano Syria na ushirikiano wa kijeshi dhidi ya makundi ya siasa kali
nchini Syria.
Msemaji
wa Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani, John
Kirby, amesema uamuzi huo unatokana na kushindwa kwa Urusi kuheshimu ahadi zake, na pia kutoonesha nia ya kuulazimisha
utawala wa Syria kutekeleza mambo
ambayo awali Urusi ilikuwa
imeyakubali.
Taarifa
ya Marekani juu ya kusitishwa kwa
mazungumzo hayo na ushirikiano na Urusi iliyotolewa inagusia pia mashambulizi makali dhidi ya
maeneo ya kiraia, miundombinu na hospitali katika mji wa Aleppo.
Na, Mhariri
Twimanye Chanzo DW.
KIMATAIFA.
Shirika
la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF,
na Benki ya Dunia wanasema kuwa watoto milioni 385 duniani wanaishi kwenye ufukara wa kutisha.
Taarifa
iliyotolewa na taasisi hizo za kimataifa inasema watoto
kwenye maeneo ya Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara na kusini mwa Asia,
hasa India, ndio walio kwenye hali mbaya zaidi.
Mwaka
2013, ilikisiwa kuwa asilimia 19.5 ya
watoto kwenye mataifa yanayoendelea walikuwa wakiishi kwenye familia ambazo
zilikuwa zinapata dola 1 na senti 90 pekee za Kimarekani kwa siku, kwa mujibu wa
ripoti hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa UNICEF, Anthony Lake,
anasema watoto wadogo ndio wenye kuumizwa zaidi na ufukara huo,
unaodumaza ukuwaji wao wa kiakili na kimwili.
Na, Mhariri
Twimanye Chanzo
DW.
MISHO WA TAARIFA YA HABARI
Post a Comment