0

TAARIFA YA HABARIKUTOKA RADIO SENGEREMA FM.



      TAMKO   LA  RAIS
Rais Dkt, John Pombe Magufuli amewataka wanasiasa nchini  kutotumia  siasa katika maafa ya Kagera yaliyotokana na tetemeko la ardhi,  na badala yake  waungane  kutoa midaada  ya hali  na  mali   kwa waathirika .

Rais Dkt ,Magufuli   ameyasema hayo ikulu jijini Dares salam wakati waziri wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa kassim Majaliwa Kassim  akimpa taarifa ya maafa  yaliyotokana na tetemeko la ardhi Mkoani  Kagera na kuwataka wanasiasa nchini    kutotumia maafahayo kisiasa.


Pia Rais ametoa onyo kwa watu  wote wasiokuwa  na mapenzi mema  wanaotumia maafa  hayo ya kagera kukusanya fedha kutoka kwa  watu mbalimbali , na kuvitaka vyombo vya  dola  kuingia kazini na kuwakamata wahusika wote aliyowaita matapeli.

Katika hatua   nyingine   Rais Magufuli  ametoa  wito   kwawananchi  wa   kagera  kutobweteka na kusubiri  misaada  ya serikali na kuwataka kujipanga kufanya kazi na kwamba serikali  itafanya yale  yaliyondani ya uwezo wake.

Na,   Mhariri  Twimanye  Chanzo                                     ITV.


                                                GEITA 
Wasamaria wema kwa  kushirikiana na  jeshi la jadi sungusungu kata ya Kalangalala halamashauri ya mji wa  Geita   wamemtia mbaroni kijana anayedaiwa kukutwa katika     nyumba ya kulala wageni akifanya mapenzi na mwanafunzi wa kidato cha nne.
Mwaandishi  wetu   YOSEPH  MASOTA kutoka Mkoani Geita anaarifu.
kijana huyo philibert juliasi(26)mkazi wa kijiji cha kayenze alikamatwa saa 4:30 usiku akiwa na mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16 wa kidato cha nne(jina tunalihifadhi) shule ya sekondari mwatulole.
Baada kukamatwa julias pamoja na mwanafunzi huyo walifikishwa  ofisi ya sungusungu,na ikawa hivi wakati wakihojiwa na katibu wa sungusungu abeli richard.
kwa upande wake mtuhumiwa alidai kuwa alianza kufahamiana na binti huyo baada ya kwenda kwake kurusha muziki kwenye simu,na hadi anakamatwa alikuwa hajui kama ni mwanafunzi.
mama mzazi wa mwanafunzi huyo,fortunata chambala anasema mtoto wake alitoweka nyumbani katika mazingira ya kutatanisha tangu jumatatu iliyopita hadi alipopata taarifa za mwanae kukamatwa gesti.
 licha ya serikali kutilia mkazo suala la elimu sanjali na kuwachukulia hatua wanaokwamisha mkazo huo,baba mzazi wa mtoto charles pastory akaomba suala hilo lisifikishwe kwenye vyombo vya sheria badala yake kufanyike mazungumzo,hali ambayo ilipingwa na katibu wa sungusungu ambaye aliita askari polisi ili kumchukua mtuhumiwa huyo.
mwandishi wa habari hizi alishuhudia askari polisi wa wilaya ya geita,wakiondoka na mtuhumiwa pamoja na mwanafunzi huyo kwa ajili ya kwenda kuwachukua maelezo kwa hatua zaidi za kisheria.
 Na,  Yoseph masota /Mhariri  Twimanye  chanzo     Tukio.

                                       PAMBA.
Wakulima wa zao la pamba katika kijiji cha NGOMA wilaya ya Sengerema mkoa wa MWANZA Wameiomba serikali  kurudisha mizani ya zamani ya Lula kwani   iliopo kwa sasa   wamedai kuwa inawapunja.
Mwanahabari wetu  Said  Mahela   anahabari   kamili.
Kauli hiyo imetolewa   na  wakulima wa  pamba    kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na diwani wa kata hiyo  mh,ONESMO MASHILI   ambapo wamesema kuwa,       uwepo wa mizani hiyo imewakatisha tamaa kulima zao hilo.

MH, Mashili ambaye ni diwani wa kata ya ngoma ameiomba serikali kutatua tatizo la  kubadilishwa kwa  mizani  inayotumika kwa sasa katika kata yake ama itoe semina juu ya utumiaji wa mizani hiyo kwa wakulima wa pamba ili   wawe na uelewa wa kutumia mizani mipya iliyopo.
 Kwa upande wake  LAZARO CHUMU Afisa mtendaji wa kata hiyo amewaomba wakulima wa zao la pamba kununu mbegu iliyo bora na serikali inatalajia kutoa mbegu kuanzia  Novemba 15 mwaka huu.


Hata hivyo  , amewaomba wakulima kuandaa mashamba yao  mapema  kwani msimu  wa kilimo  umekaribia.

                       TAASISI.  
Waziri wa afya maendeleo ya jamii ,jinsia wazee na watoto  Ummy Mwalimu ameyataka mashirika yasio ya kiserikali kufanya kazi kwa mujibu wa usajiri wake, badala ya kujiingiza katika masuala ya siasa. 
Waziri Ummy mwalimu ametoa kauli hiyo  katika mkutano wake na bodi ya uratibu   wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali  ambapo amesema kuwa zipo  tarifa za kuwepo kwa baadhi ya mashirika hayo kujihusisha na masuala ya kisiasa.             
Awali mwenyekiti wa bodi hiyo Nichorus Zacharia ameiomba serikali kusimamia taasisi binafsi zinazoenda    kinyume cha maadili zifutwe.
Na,  mhariri    Twimanye   chanzo   TBC.



                    KIMATAIFA.
Serikali ya Sudan Kusini  imekanusha madai ya ufisadi yaliyotolewa kwenye ripoti ya shirika moja la Marekani kwamba madai hayo ya ufisadi , miongoni mwa maafisa wa ngazi ya juu nchini humo wanayumbisha pia mchakato wa amani wa nchi hiyo.

Ripoti hiyo inaeleza jinsi vigogo wanavyojilimbikizia mali huku wananchi wa kawaida wakiteseka kutokana na madhila ya vita.

Msemaji wa rais Salva Kiir, anasema madai hayo hayana msingi wowote na kuwa mataifa ya magharibi yanataka kuchochea mapinduzi ya serikali yake.

Na,   Mhariri  Twimanye  chanzo      BBC.


                 KIMATAIFA
Serikali ya Zimbabwe imewaonya waandamanaji  wasishiriki  kamwe   maandamano kwenye mji mkuu Harare.
Waziri wa mambo ya ndani amesema kuwa vikosi vya usalama vitalinda kwa  ukamilifu  amani ya nchi hiyo.
Polisi wametoa onyo wakisema kuwa wale watakaokamatwa kwa kushiriki maandamano hayo watafungwa hadi mwaka mmoja.

Kumekuwa na maandamano ya kila mara miezi ya hivi karibuni nichgini  Zimbabwe  yanayotaka kufanywa mabadiliko katika upigaji kura na kuondolewa madarakani kwa Rais Robert Mugabe.
Na,  Mhariri   Twimanye                Chanzo    BBC.


NA HUO NDIO MWISHO WA TAARIFA YA HABARI  KUTOKA RADIO SENGEREMA FM.


KWA TAARIFA NYINGINE YA HABARI USIKOSE KUJIUNGA NASI  KESHO SAA KUMI    KAMILI JIONI.















Next
Newer Post
Previous
This is the last post.

Post a Comment

 
Top