BUNGE
Halmashauri zote nchini zimetakiwa kutenga maeneo mbadala yanayopitika na yanayofaa kwa ajiri ya wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga ili kuwaondolea usumbufu wanaoupata.
Waziri ofisi ya Rais Tamisemi utumishi na utawala bora George Simbachawene akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na mbunge wa jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula ambapo alihoji je serikal iko tayari kupitia wizara ya tamisemi kuzisaidia kifedha halmashauri ili kuweza kuboresha maeneo yawe rafiki kwa wafanyabiashara Simbachawene amesema serikal imekwishatenga million 350 kwa ajiri ya ujenzi wa miundo mbinu hiyo.
Hata hivyo Simbachawene amewataka wafanyabiashara hao wadogo wadogo kuepuka usumbufu wa kufanyia biashara pembezoni mwa barabara ili kuondoa msongamano wa watu na vitu vyao.
Hali kadhalika amesema miongoni mwa wafanyabiashara wanaliingizia taifa kipato ni machinga hivyo wako mbioni kutenga maeneo rafiki ili wafanye kazi zao bila usumbufu wa aina yoyote ile.
UKATIRI GEITA.
Polisi mkoani Geita imemfikisha katika mahakama ya hakimu mkazi mfawithi wilayani humo mkazi mmoja wa kijiji cha Bugela Bw. Wambula kiginga kwa kosa la kumnajisi mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka 9.
Mwandishi wetu AMINA HASANI anataarifa zaidi.
Akisoma shitaka hilo mwendesha mashitaka wa polisi Samini Mzigo,amesema kwa nyakati tofauti kati ya mwezi January mwaka huu hadi octobar mwaka huu majira ya usiku mshitakiwa wambula alikuwa akimbaka mtoto wa mke wake jina limehifadhiwa.
Baada ya kuhojiwa na hakimu wa mahakama hiyo Jovitha Katto,mshitakiwa amekana shitaka hilo na kesi yake imepangwa kusikilizwa November 11 mwaka huu ambapo kwa upande wa jamhuri ya muungano imejipanga kuwasilisha mashahidi .
Hata hivyo kutokana na uzito wa kesi hiyo mahakama imeamuru kuweka zuio la dhamana kwa mshitakiwa Wambura.
MRADI WA MAJI SENGEREMA
Kufuatia kauli ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt JOHN POMBE MAGUFULI kuwa ifikapo desemba mwaka huu mradi wa maji safi na usafi wa mazingira LVWASTAN II uliopo sengerema uwe umekamilika, huenda usikamilike kwa muda huo.
Hayo yamebainika wakati wadau wa mradi huo MSF walipotembelea mradi huo katika chanzo cha maji Nyamazungo na kubaini mapungufu makubwa yaliyopo ndani ya mradi huu na kuomba mapungufu hayo yafanyiwe utekelezaji haraka.
Upande wake msimamizi wa mradi huo bw. Gogad mgwatu na mshauri mkuu wa mradi huo bw,Adam Ludovick wamekiri kuwa mradi huo huenda usikamilike kwa wakati kutokana na kutokuwepo na fedha za kutosha na ucheleweshwaji wa vifaa vya ujenzi wa mradi huu.
MAHINDI
Zaidi ya Hekari 30 za wakulima zilizolimwa zao la mahindi katika kijiji cha Kang’washi Wilayani Sengerema, zimenyauka kwa jua baada ya kukosa mvua na kuzua hofu kwa wakulima ya kukubwa na baa la njaa.
Wakulima wa eneo hilo wamesema kutokana na mvua kuadimika mara baada ya kuanza kwa msimu wa kilimo, hali hiyo imesabababisha mahindi waliyoyalima shambani kuanza kunyauka.
Wamesema kufuatia hali hiyo sasa wameanza kupata taharuki miongoni mwa wakulima.
Katika kukabiliana na hali hiyo wakulima hao wameiomba serikali kuwapelekea mbegu zinazostahimili ukame ili waweze kukabiliana na hali hiyo iliyoanza kujitokeza mwanzoni mwa msimu wa mvua.
Bi LEAH RICHARD KACHWELE ………… ni Mwenyekiti wa eneo la Shuleni katika Kijiji Cha Kang’washi Wilayani Sengerema ambaye anasema hali hiyo ya kukosa mvua imesababisha viongozi wa kijiji kupata hofu ya kukumbwa na baa la njaa huku akisema watafanya mikutano ili kulitafutia suluhu suala hilo.
Wakati suala la kuadimika kwa mvua likiwanyima usingizi wakulima wa kijiji hicho, tayari mamlaka ya hali ya Hewa nchini( TMA) imetangaza mvua za mwaka huu zitakuwa za wastani na hivyo kuwataka wakulima kuchukua tahadhari ya kulima mazao yanayostahimili ukame.
Wizara ya Mashauri ya Kigeni imesema kuwa utaratibu wa kumuachisha kazi Jemedari Johnson Mogoa Kimani Ondieki haukuwa na uwazi.
Katibu Mkuu wa UN Ban Ki-moon alimfuta kazi Luteni Kanali Johnson Ondieki baada ya ripoti ya uchunguzi kusema alikosa kuwajibika kulinda raia mapigano yalipozuka upya nchini Sudan Kusini mwezi Julai.
Ripoti hiyo imesema walinda amani waliokuwa chini ya jemedari huyo hawakuchukua hatua yoyote wanajeshi wa serikali waliposhambulia kituo cha utoaji misaada mjini Juba na kuwadhulumu raia.
Kenya imesema uamuzi huo si wa haki na kutangaza kwamba itayaondoa mara moja majeshi yake yanayohudumu chini ya UN nchini Sudan.
Kadhalika, Kenya imejiondoa kutoka kwa mpango wa kutuma wanajeshi wa ziada kutoka nchi za kanda ambao walitarajiwa kutumwa kuimarisha kikosi cha UN nchini humo.
KIMATAIFA.
Wakati vikosi vya Iraq vikizidi kuusogelea mji wa Mosul, kiongozi wa wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS Abu Bakr al-Baghdadi amewatumia ujumbe wa sauti wapiganaji wake akiwataka kutosalimu amri dhidi ya majeshi ya serikali.
Kiongozi huyo amesikika akisema hakuna kusalimu amri na kuwaambia wapiganaji kwamba ni heshima kuilinda ardhi hiyo kuliko kusalimu amri kwa aibu.
Huo ni ujumbe wa kwanza kutolewa na kiongozi katika kipindi cha mwaka mmoja na kumekuwa na tetesi juu ya afya na harakati za kiongozi huyo lakini hajulikani alipo.
Mwezi Juni mwaka 2014, alijitokeza hadharani mjini Mosul na kutangaza Dola la Kiislamu nchini Iraq na Syria.
Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani na unaoviunga mkono vikosi vya Iraq, unakadiria kuwepo kiasi ya wapiganaji 3000 hadi 5000 wa IS ndani ya mji wa Mosul.
MICHEZO NA BURUDANI
Ushindi wa mabao 2-1 walioupata Mbeya City dhidi ya Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, jana unakuwa mtihani mwingine kwa Yanga.
Yanga wanaingia kwenye mtihani huo kutokana na mechi inayofuatia dhidi ya Prisons ambao wanakutana nao Jumamosi.
Prisons ambao wanashindana kwa juhudi zote na Mbeya City, hawatakubali kuona wao wanaishindwa Yanga kwa mambo mawili.
======= =======
Baada ya kuitwanga Stand United iliyokuwa haijawahi kufungwa kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga msimu huu, Simba imenogewa na pointi.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema wanataka kumalizia mechi mbili zilizobaki za mzunguko wa kwanza kwa ushindi pia.
Simba ndiyo vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 35 kileleni, tofauti ya pointi nane na Yanga wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 27.
===== ====== ======
BIASHARA
Baada ya harimashauli ya wilaya ya Sengerema kutoa mashine za kielectronic za kukusanyia mapato,Hali ya mapato imeongezeka ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Akizungumza kwa niaba ya mkurungenzi Afsa Tehama wa wilaya Bwn,MAGEMBE EDWARD amesema hali hii imekuja baada ya kutoa mashine za kukusanyia mapato kwa kila sehemu yenye vyanzo vya mapato ndani ya harimashauli.
Aidha amebainisha kuwa jumla ya mashine sitini (60) za kielectronic zilizo nunuliwa na harmashauli tayali mashine Hamsini na nane(58) zimeshatolewa kwenye maeneo tofauti na mbili kubaki makao makuu .
Hata hivyo amesema baadhi ya changamoto wanazo kumbana nazo ni mashine kugoma kutoa lisiti ya mlipaji kutokana na miundo mbinu ya mitandao kuferi.Na hivyo tayali wamesha anza kukabiliana na changamoto hizo.
Bwn MAGEMBE pia amesema kuwa yeyote atakae bainika kukusanya mapato kwa kutumia vitabu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Post a Comment