0
                    

       WIZI WA DAWA
Mfamasia wa Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza Bw,KENETH JOHN MAYENGO amekamatwa na jeshi la polisi kwa  tuhuma ya kuiba na kusafilisha dawa kinyume na sheria.

Akithibitisha tukio hilo mkuu wa wilaya ya sengerema Bw,EMMANUEL KIPOLE amesema dawa hizo zilichukuliwa na mfamasia huyo jana majira ya saa saba katika stoo ya dawa na kumkabidhi dereva  bodaboda kwa ajili ya kwenda kuziuza.
Redio sengema imemtafuta mkurugenzi wa wilaya ya sengerema Bw,MAGESA  MAFULU BONIFASI ambae ni mwajili wake  na kueleza kusikitishwa na kitendo hicho..
                                       ZIARA.
Waziri wa kilimo mifugo na uvuvi ambaye pia ni mbunge wa jimbo la buchosa Dkt. Charles Tizeba ameahidi kutekeleza ahadi yake ya kujenga zahanati kila kijiji kama alivyoahidi kipindi cha uchaguzi kabla ya kukamilika kwa miaka yake mitano kumalizika.

Kauli hiyo ameitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Luholongoma kata ya Kafunzo halmashauri ya Buchosa.
Katika kufanikisha ujenzi huo wa zahanati amesema atashirikiana na wananchi ambapo wao watachangia mchanga na kokoto ambapo yeye atahakikisha anakamilisha ujenzi huo wa zahanati.
Tizeba amesema amechoka kuona wananchi wakihangaika kutafuta huduma za afya umbali mrefu hivyo atahakikisha anakamilisha ili kuwaondolea adha wananchi.
                                  MISITU
Kikosi cha Kufuatilia na Kuzuia Uharibifu wa Misitu cha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kimefanikiwa kukamata lori lenye namba za usajili T 676 ANQ lililokuwa likisafirisha mbao kinyume cha sheria huku zikiwa zimefichwa kwa kufunikwa na bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Kaimu Afisa Habari wa Wakala huyo, Nurdin Chamuya amesema baada ya kupata taarifa hizo vikosi hivyo vilifika eneo la tukio na kufanya mahojiano ambapo mmoja kati ya wahudumu wa lori hilo alieleza kuwa lori hilo lilitokea Mkoani Kigoma na kwamba lilikuwa limepakia mzigo wa sabuni na chupa za maji zilizotumika.

Chamuya ametoa wito kwa wananchi wote nchini kushirikiana na Serikali katika uhifadhi na ulinzi wa rasilimali za misitu na kuacha fikra potofu kuwa kazi hiyo ni ya Serikali pekee na taasisi zake kwakuwa faida zake hunufaisha jamii yote.
                                     MSAADA

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala ameipongeza idara ya Afya Wilayani Kakonko kwa jitihada ya kupungua kwa vifo vya mama na mtoto kutoka vifo 404 Kati ya vizazi hai 100,000 kwa mwaka kutokana na wadau wa Afya kuchangia Huduma hiyo kwa ushiriki wa pamoja na watumishi wa idara ya afya.

Kauli hiyo imetolewa wakati mkuu huyo akipokea msaada wa vitanda Na magodoro 18 kutoka katika kampuni ya taasisi za kifedha NMB Kanda ya magraribi Tabora tawi la Kakonko lengo likiwa ni kuchangia kupunguza vifo vya mama Na Mtoto katika wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma.

Ndagala amesema jitihada zinazofanywa na wadau pamoja na idara ya afya zinaonyesha wazi kuwa vifo hivyo vitazidi kupungua siku hadi siku.


Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameipongeza Benk hiyo kwa msaada ulioutoa katika hospital ya wilaya na kuwaomba watumishi na wananchi kuvilinda vitanda Na magodoro yaliyotolewa kuweza kusaidia Wananchi Na Serikali kwa ujumla ili kuweza kupunguza ukosefu wa vitanda.

                             KIMATAIFA       
Wakuu wa Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways, wanasema shirika hilo limepunguza kwa kiwango kikubwa hasara ambayo shirika hilo limekuwa likipata, na kuibua matumaini kwamba huenda shirika hilo likajikwamua.

Matokeo ya kifedha yaliyotangazwa na Mkurugenzi wa kifedha wa shirika hilo Dick Murianki yanaonesha shirika hilo lilipata hasara ya Sh bilioni 4.73 kabla ya kulipa ushuru kipindi cha miezi sita hadi kufikia tarehe 30 Septemba.

Huku ni kuimarika kwa  asilimia 60% ukilinganisha na hasara ya Sh bilioni 11.86 ambayo shirika hilo lilipata kipindi sawa na hicho mwaka 2015.
Afisa mkuu mtendaji wa shirika hilo Mbuvi Ngunze amesema kuna matumaini kwamba shirika hilo litajikwamua.
         
MICHEZO NA BURUDANI
Kocha Joseph Omog amewataka wachezaji wake kuamka na kuhakikisha wanatumia nafasi wanazozipata.

Simba imekuwa moja ya timu zinazopoteza nafasi nyingi za kufunga mabao katika mechi za Ligi Kuu Bara.
Omog raia wa Cameroon ambaye mara kwa mara amekuwa akiwasisitiza wachezaji wake kuzitumia nafasi sasa ameamua kuweka msisitizo.

Simba inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 29 baada ya kucheza mechi 11 huku Yanga ikiwa na pointi 24 baada ya mechi 11 pia.
            =======      =======   =======
Katika ndondi,
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah PaziDulla Mbabe’ kesho anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na  Mchina, Chengbo Zheng katika pambano lisilokuwa la ubingwa ambapo amefunguka kuwa  kichapo  atakachompa hakitokuwa cha kawaida kwa upande wake kutokana na maandalizi aliyoyafanya.
==========       =========     ========
Nako barani uropa, Droo ya Mechi za Robo Fainali ya EFL CUP, Kombe la Ligi la England, imefanyika jana mara baada ya Mechi ya mwisho ya Raundi ya 4 ambayo Man United iliwabwaga Mabingwa Watetezi wa Kombe hili Man City 1-0 huko Old Trafford.

Katika Droo hiyo, Vigogo wote wa Ligi Kuu England waliobakia kwenye Mashindano haya wamepangwa kucheza Mechi zao Viwanja vya Nyumbani kwao na hiyo ni faida kubwa kwao.
                         =====   ======    ======







Post a Comment

 
Top