TAARIFA YA HABARI KUTOKA RADIO SENGEREMA
UHALIFU
Vijana katika kijiji cha Nyanguku kilichopo kata ya Nyanguku
wilaya ya Geita mkoani Geita, wametakiwa kufanya kazi kwa
bidii ili kuepukana na vitendo vya uhalifu.
Taarifa
na mwanahabari wetu PETE KADASHI.
Hayo yamesemwa na
viongozi wa kijiji hicho katika mkutano uliofanywa kwa ajili ya kubaini wezi
wanaoiba mali za wakazi wengine.
Katika Mkutano
huo mwenyekiti wa kijiji cha
Nyanguku pamoja na mtemi wa jeshi la jadi maarufu kama sungusungu wamesema,
wizi unaofanyika ni ule unaofanywa majumbani wakati wa usiku.
Baadhi ya wanakijiji
waliopata fursa ya kuzungumza na redio sengerema wamewaomba vijana
kujishughulisha na kilimo ili kuondokana na uharifu kwa ajili ya usalama wa
mali za wengine.
Mkutano huo uliofanyika
katika kitongoji cha Bujingwa kijiji
cha Nyanguku, umewabaini watu saba
ambao wadaiwa kuwa
na tabia ya kufanya uhalifu na kupigwa
faini ya shilingi 125,000 kwa kila mmoja
.
Na,
Mashamba /Mhariri Twimanye Chanzo: Mkutano.
MAENEO YA MAZIKO
Wananchi wilayani
Sengerema Mkoani Mkoani wameitaka halmashauri ya Wilaya ya
Sengerema kutenga maeneo mapya
ya maziko kutokana na maeneo
ya awali kujaa kwa muda mrefu bila kupatiwa ufumbuzi.
Wananchi wamesema kujaa kwa sehemu ya maziko kwa baadhi ya maeneo hali hiyo
imesababisha adha kubwa pindi wanapokwenda kuhifadhi miili ya wapendwa
wao ikiweko kukutana na mifupa ya binadamu waliozikwa zamani.
Hata hiyo wamesema halmashauri ya sengerema ishughulikie
suala hilo mapema ili kuondoa usumbufu kwa wananchi kuhangaika
kutafuta mahali pa kuwahifadhi wapendwa wao.
Chanzo:Mahojiano.
UKATILI.
Jamii yatakiwa kuwafichua
watu wanaofanyia vitendo vya
ukatili wa kijinsia
akinamama ,wasichana na
watoto ili kutokomeza vitendo hivyo hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa
na Afisa ufuatiliaji
na tathimini kutoka shirika la Kivulini linalojihusisha na kutetea haki za
wanawake na wasichana lililopo
Mkoani Mwanza Bwn,Mathias Shimo wakati akitoa mafunzo
kwa wadau mbalimbali dhidi ya kupinga
ukatili katika ukumbi wa mikutano
Telecentre.
Kwa upande wao
baadhi ya wadau waliopatiwa
mafunzo hayo wamelishukuru shirika hilo na kuahidi kwenda kuyafanyia
kazi yote waliofundishwa katika maeneo yao ili kuhakikisha vitendo vya ukatili
dhidi ya akinamama,wasichana na watoto vinapungua .
Shirika la Kivulini lenye makao yake makuu Mkoani
Mwanza limezindua kampeni ijulikanayo kwa jina la TWAWEZA hivi karibuni yenye lengo la kupinga ukatili wa kijinsia .
Na,Mhariri
Twimanye Chanzo Mahojioano.
UZINDUZI WA MADAWATI
Naibu waziri wa maliasili na utalii Eng,
Lwamo Makani amezindua ugawaji wa madawati elfu ishirini yanayotolewa na wakala wa misitu nchini TFS Mkoani Mwanza .
Awali kaimu mkurugenzi wa
wakala wa misitu hapa nchini TFS Bwn, Dosantos Silayo amesema kuwa
wamefanikiwa kutengeneza madawati 12,115
sawa na asilimia 61 na kwamba baadhi ya mashamba ya misitu yalichelewa kuvunwa na kusababisha kuchelewa kukamilisha
asilimia 39 iliyobaki.
Akizindua ugawaji wa madawati hayo Eng. Makani amegawa madawati 2,580
kati ya madawati 12,115
yaliyotayari kwa mikoa ya
kanda ya ziwa ,Mwanza , Geita,Kagera,
Simiyu na Mara huku kiasi
kilichobaki kikitazamiwa kutolewa kwa
mikoa mingine hapa nchini.
Eng. Makani amesema kuwa kutekelezwa kwa mpango huo
kumetokana na rasilimali mistu ambayo nayo inapaswa kutunzwa na wananchi wote.
Na,Meshack/Mhariri Twimanye Chanzo Uzinduzi.
KIMATAIFA.
Majaji wa kesi za uhalifu wa kivita mjini The Hague wamemhukumu kifungo cha miaka
tisa gerezani aliyekuwa mwanamgambo wa itikadi kali aliyekiri kuyaharibu maeneo
takatifu wakati wa mgogoro wa Mali
mwaka wa 2012.
Hii ni kesi ya kwanza ambayo imelenga uharibifu wa turathi za
kitamaduni.
Makundi ya kutetea haki za binaadamu na watalaamu wa
kimataifa kuhusu masuala ya sheria wanasema
kuwa, kesi dhidi ya Ahmad al-Faqi al-Mahdi katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai huenda
ikasaidia kuzuia uharibifu wa aina hiyo unaoendelea kuigubika migogoro ya kimataifa
bila kuchukuliwa hatua za kisheria.
Al-Mahdi ameelezea masikitiko yake kutokana na kuhusika kwake katika
uharibifu wa nyumba 10 za makaburi na maeneo ya kidini mjini Timbuktu ambayo yalijengwa katika karne
ya 14 nchini Mali.
Na,Mhariri
Twi manye Chanzo Dw.
Taarifa kutoka nchini
Marekani zinaeleza kuwa Treni
moja imegonga kituo cha reli kwenye mji wa Hoboken
ulio jimbo la New Jersey nchini humo.
Idara inayohusika na
huduma za dharura jimba la New Jersey
inaripoti kuwa watu watatu wameuawa na zaidi ya 100 kujeruhiwa .
Picha kwenye mitandao ya
kijamii zinaonyesha uharibifu mkubwa katika treni
hiyo na kituo.
Kituo cha Hoboken kipo umbali ya maili saba kutoka mji wa New York na watu wengi hukitumia
kusafiri kwenda mtaa wa Manhattan.
Ben Fairclough ambaye alikuwa eneo hilo anasema kuwa
treni hiyo ilikuwa imetoka kwenye njia yake.
Na, Mhariri Twimanye
Chanzo Dw.
PATO
Pato la
Taifa limeendelea kukua kwa asilimia 7.9 katika kipindi cha mwezi Aprili hadi
Juni mwaka huu ikilinganishwa na kasi ya asilimia 5.8 katika
kipindi cha mwaka uliopita.
Takwimu hizo
zimetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa
ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu hali ya pato la Taifa kwa robo ya pili kuanzia
Aprili hadi Juni mwaka huu.
Dkt Chuwa amesema kuwa ukuaji wa pato la Taifa umetokana na shughuli za
kiuchumi ikiwemo kilimo, mifugo, misitu na uvuvi ambapo shughuli hizo
zilikuwa kwa asilimia 3.2 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 1.9 katika
kipindi cha mwaka uliopita.
Kwa upande wa
shughuli za uchumi za viwanda na ujenzi, Dkt. Chuwa amesema
kumekuwa na ongezeko la asilimia 20.5 katika kipindi hicho ukilinganisha na
ukuaji wa asilimia 11.2 mwaka 2015 katika shughuli za uchimbaji madini, mawe na
kokoto.
Aidha katika
shughuli za uzalishaji bidhaa na viwanda kumeongeza kwa asilimia 9.1 katika
kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 ukilinganisha na kasi ya asilimia 5.2 ya
mwaka 2015.
Na, Mhariri Twimanye
Chanzo Michuzi
Post a Comment