VYOO BORA
Mkuu
wa Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza Bwn,Emmanuel Kipole ametangaza kiama kwa wananchi ambao hawajajenga
vyoo vya kudumu katika
makazi yao.
Katika
mahojiano na Radio Sengerema Bwn,Kipole amesema kuwa kaya nyingi hazina vyoo bora hasa katika maeneo ya mjini, hali ambayo inapelekea wananchi kujisaidia
ovyo na amewagiza viongozi wote
kuhakikisha kila kaya inajenga choo.
Ameleza
kuwa awali kulikuwa na ulegevu wa sheria juu ya ufuatiliaji wa suala la ujenzi wa vyoo , lakini kwa sasa watatembelea kaya moja hadi nyingine ili
kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo cha kudumu ili kuepuka magojwa ya
milipuko.
Hata
hivyo Bwn,Kipole amebainisha kuwa kwa yeyote atakae kaidi kujenga choo
cha kudumu hatua kali za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake ikiwemo kupelekwa mahakamani kwani watu wachache
wazembe hawawezi kusababisha Wilaya nzima
ya Sengerema kukumbwa na magonjwa ya milipuko.
MTIHANI
Jumla
ya watahiniwa 408,442 wa kidato cha nne wanatarajia kuanza mitihani ya kidato
cha nne itakayoanza kesho, ikiwa ni idadi pungufu ya waliofanya mtihani huo
mwaka jana.
Akizungumza
na wanahabari leo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Dk Charles Msonde amesema mwaka jana
kulikuwa na watahiniwa 448,382 waliofanya mitihani huo.
Dk Msonde
amesema maandalizi yote ya mitihani hiyo itakayomalizika Novemba 18, mwaka huu
yameshakamilika.
Kawa
wake Afisa Elimu Sekondari Wilayani Sengerema Mwl GODWINI BALONGO amewataka wanafunzi wote wa kidato cha Nne
kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote ili kuepuka kufutiwa matokeo.
MAHAKAMANI.
Mtu mmoja
amefikishwa katika mahakama
ya wilaya ya
sengerema mkoani mwanza
kwa tuhuma ya
ubakaji.
Taarifa zaidi na mwandishi wetu JOYCE ROLLINGSTONE
alifika mahakamani hapo.
Akisoma shitaka
hilo mbele ya
hakimu wa mahakama
hiyo BI MONIKA NDYEKOBORA mwendesha
mashitaka wa jeshi
la polisi INSPECTA SLIVESTA
MWAISEJE amemtaja
mshitakiwa kuwa ni
ALPHONCE DEUSI mwenye umri
wa miaka 18 mkazi
wa NYAMLEGE KATUNGURU.
INSPECTA
MWAISEJE
amesema kuwa mshitakiwa
anashitakiwa kwa kosa
la kubaka kinyume
na kufungu 130
na 131 cha
kanuni ya adhabu
kuwa mnamo octoba
23 mwaka huu
majira ya saa
3:00 usiku eneo
la katunguru alimbaka
msichana ambaye jina
lake limehifadhiwa mwenye
umri wa miaka
16 mwanafunzi wa
sekondari kidato cha
pili .
Hata hivyo
mshitakiwa amekana kutenda
kosa hilo,na yuko nje
kwa kutimiza mashaliti
ya dhamana hadi NOVEMBA
14 mwaka huu
kesi hiyo itakaposikilizwa tena
mahakamani hapo.
MAZINGIRA
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepiga marufuku uharibifu
mkubwa wa mazingira unaendelea katika maeneo mbalimbali nchini ambao unaweza
kusababisha nchi kugeuka jangwa.
Makamu wa Rais ametoa
kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua
mkutano kimataifa unaohusu mabadiliko ya tabia ya nchi unaokutanisha
wanasayansi, watafiti na wadau wa mazingira chini ya Usimamizi wa Kigoda
cha mwalimu Julius Nyerere cha Mazingira na mabadiliko ya Tabia ya nchini
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Makamu wa Rais ameonya
kuwa jukumu la kuhifadhi mazingira sio la Serikali peke yake bali ni kila
mwananchi na wadau wa mazingira kwa ujumla, hivyo wananchi ni muhimu kwa umoja
wao wakaongeza jitihada za kupanda miti katika maeneo yao ili kukabiliana na
hali tete ya uhabifu wa mazingira nchini.
Makamu wa Rais
ametahadharisha kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yameanza kuleta athari si kwa
Tanzania na dunia kwa ujumla hivyo jitihada za makusudi zinahitajika ili
kuhakikisha changamoto zinazojitokeza kwa sasa zinakabiliwa ipasavyo.
AGIZO
Mkuu wa
wilaya ya uvinza mkoani Kigoma bw Mwanamvua Mlindiko amewataka viongozi wa serikali za vijiji
wilayani humo kutowapokea wageni kutoka nchi jiarani wanaoingia katika vijiji
hivyo kwa ajiri ya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na uvuvi kutokana na
kuogopa kuhatarisha usalama.
Mkuu huyo
wa wilaya ametoa agizo akiwa katika ziara yake kwenye vijiji vya mwambao wa
ziwa Tanganyika ambavyo vimepakana
na jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
baada ya taarifa za kuwepo kwa wageni na wahamiaji wanaoingia na kuishi katika vijiji hivyo
kinyume cha sheria hali ambayo imekuwa ikiongeza vitendo vya uharifu.
Kwa upande
wao wananchi wamesema tatizo kubwa katika vijiji hivyo ni pamoja na kuingia
wageni kutokana na serikali kutoajiri maafisa watendaji wa vijiji na kata hali
iliyosababisha nafasi hizo kukaimiwa na watu wasiokuwa na uwezo nazo.
Mwenyekiti
wa halmashauri wa wilaya ya Uvinza
Jackson Mateso ameeleza kuwa
shuguli za uvuvi zinazotegemewa na wananchi hao zimeendelea kuboreshwa licha ya
kuwepo matatizo ya upungufu wa maafisa Uvuvi wilayani humo.
Afisi ya bwana Ban imesema kuwa inathamini jukumu la taifa hilo katika kupigania
haki na kwamba inatumai taifa hilo litaangazia upya uamuzi wake.
Afrika
Kusini
imesema mapema mwezi huu kwamba itajiondoa katika mahakama ya ICC kwa sababu ni
kikwazo katika juhudi zake za kukuza amani barani Afrika.
Mwaka uliopita ,mahakama ya Afrika Kusini
iliikosoa serikali kwa kukataa kumkamata rais wa Sudan Omar El bashir.
moon
Mataifa ya Burundi na Gambia tayari
yametangaza kujiondoa katika mahakama hiyo.
KIMATAIFA
Ripoti ya shirika la Umoja
wa Mataifa linalowahudumia watoto-UNICEF inasema watoto milioni 300 kutoka kila
pembe ya dunia wanaishi kwa kuvuta hewa chafu kupita kiasi.
Vijana,wake kwa waume katika
eneo la kusini mwa Asia,Mashariki ya kati na Afrika sawa na wenzao wa Mashariki
mwa Asia na eneo linalopakana na
bahari ya Pacific ndio wanaoathirika
vibaya sana na hali hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti
hiyo,kila mtoto mmoja kati ya saba wa dunia hii anakabiliana hewa chafu,hewa
ambayo imepindukia mara sita au zaidi kile kiwango kilichowekwa na shirika la
afya la Umoja wa Mataifa WHO.
Duru nyengine za shirika la UNICEF zinasema jumla ya vijana bilioni
mbili wa dunia wanavuta hewa ambayo si safi kuambatana na vipimo vya shirika la
afya la Umoja wa Mataifa-WHO.
Chanzo cha hali hiyo ni
moshi unaotoka ndani ya magari na wa viwandani,kuchomwa moto takataka za
majumbani na vumbi.
MICHEZO NA BURUDANI
Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali amefariki dunia usiku wa
kuamkia leo October 31 2016 maeneo ya Kimara jijini Dar es salaam.
Taarifa zinadai kuwa alishambuliwa na
wananchi baada ya madai ya kuitiwa mwizi.
Taarifa kutoka kwa Promota wake, Siraji Kaike amesema watu aliokuwa
anagombana nao walimwitia mwizi na wakawa wamemshambulia na kumtupa baadaye
bodaboda waliokuwa wanamjua Thomas
Mashali walimuokota na kumpeleka hospitali ambapo baadaye zilitolewa
taarifa kuwa amefariki.
======= ======= =======
HIVI karibuni, timu kadhaa zinazoshiriki Ligi ya Mpira
wa Kikapu nchini Marekani (NBA), zilianza kuonyesha nia ya kumuwania Mtanzania Hasheem Thabeet Manka.
Timu hizo zilionyesha
nia kutokana na maendeleo mazuri ya Hasheem
katika timu yake ya Grand Rapid
ambako ameendelea kuonyesha ubora wakati ikipambana katika D-League ya NBA.
Hasheem, aligoma kusaini kuzitumikia timu kubwa za mpira wa kikapu barani Ulaya katika nchi za Hispania, Ugiriki na kwingineko, akaamua kubaki D-League.
Hasheem, aligoma kusaini kuzitumikia timu kubwa za mpira wa kikapu barani Ulaya katika nchi za Hispania, Ugiriki na kwingineko, akaamua kubaki D-League.
===== ======
======
BIASHARA
SERIKALI imesema, hakutakuwa na msamaha kwa
mfanyabiashara au mzalishaji atakayeingiza sokoni bidhaa zisizothibitishwa
ubora kwa sababu atakuwa amevunja sheria.
Akifungua maonesho ya bidhaa za wajasiriamali
yaliyoandaliwa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) mjini Bagamoyo
mkoani Pwani , Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema, wanaoingiza bidhaa sokoni bila
kuzithibitisha ubora wanalihujumu soko.
Amesema kamwe serikali haiwezi kuwaonea haya
wafanyabiashara wa aina hiyo, kwa sababu lengo lao ni ovu lenye dhamira ya
kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Mwijage amesema,
Tanzania iko katika mchakato wa kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kupitia
uzalishaji wa viwandani, hivyo inahitaji wafanyabiashara na wazalishaji wa
huduma na bidhaa wenye kuthamini ubora na sio kuzalisha ilimradi.
Amesema, huu ni wakati wa wajasiriamali
nchini kuhakikisha wanafuata taratibu zinazotakiwa kuthibitisha ubora wa bidhaa
wanazozizalisha, ili wajihakikishie mazingira salama ya kibiashara.
BIASHARA
WIZARA ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
imesema kuwa mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha mafuta ya kula
yanazalishwa kutokana na mbegu zinazozalishwa nchini ili kuongeza ajira na
kuokoa matumizi ya fedha za kigeni.
Hatua hiyo inatokana na Tanzania kuwa na hali
ya hewa nzuri kwa uzalishaji mazao mbalimbali yanayozalisha mafuta, lakini
imekuwa inaagiza kiasi cha tani laki
tatu na nusu (350,000) za mafuta ghafi
kila mwaka kutoka nje ya nchi, kwa fedha nyingi za kigeni.
Ofisa Biashara Mkuu, Idara ya Viwanda Vidogo
na Biashara Ndogo kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wilfred Kahwa amesema hayo juzi wakati
alipowasilisha mada juu ya jitihada za serikali za uwekezaji kwenye sekta ya
kilimo na viwanda.
Post a Comment