MAKAMU wa Rais, Mama
Samia Suluhu Hassan ameelezea
kukerwa na vitendovya rushwa na kuwataka wanawake wajasiriamali kufichua kila
aina ya rushwa wanazoombwa na wenye mamlaka katika sekta ya biashara nchini.
Amesema hayo wakati akifungua kongamano la wajasiriamali wanawake lililoandaliwa na Mtandao
wa Sauti ya Wajasiriamali Wanawake Tanzania (VOWET) na kuhudhuriwa na wanawake
zaidi ya 500.
Amesema iwapo
wanawake wakiwafichua waombaji wa rushwa wanaokwamisha harakati zao za kusonga
mbele kibiashara, itaiwezesha serikali kuondoa kero hiyo.
Samia ameeleza
baadhi ya wanawake wanaombwa rushwa za ngono na nyinginezo na hukaa kimya bila
ya kulifikisha suala lao hilo kwa mamlaka husika ili wasaidiwe na kwamba kukaa
kimya kumechangia kuendelea kuwepo kwa kero hiyo.
Amewahakikishia
wanawake hao kuwa serikali itakuwa ikiwapa kipaumbele kwenye malipo ya fedha za
zabuni ili waweze kusonga mbele zaidi
CCM
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip
Mangula ameelezea kufurahishwa kwake kufukuzwa kwa wanachama 100 mkoani Mwanza
kwa kubainika kukisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.
Mangula amsema, wakati mikoa itaendelea kuchukua hatua, lakini pia kwa ngazi ya taifa hatua dhidi ya waliokisaliti chama zitaendelea kuchukuliwa, ikiwa ni pamoja na kuwatupilia mbali watakaojaribu kuomba nafasi za uongozi wakati wa uchaguzi wa Chama mwakani.
Mangula amewataka
vijana nchini kote hasa wasomi, kuepuka kutumiwa vibaya na wanachama
watakaokuwa wanasaka uongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa CCM unaotarajiwa
kufanyika mwakani, kwa kuwa kijana yeyote atakayekubali kutumiwa vibaya atakuwa
amekisaliti chama.
MAHAFALI
Imeelezwa kuwa watoto wa kike
wana nafasi kubwa ya kutimiza ndoto zao endapo wataamua kutoyakimbia masomo ya
sayansi kutokana na sekta ya sayansi kuwa na wigo mpana wa fursa za kuajiriwa
na kujiajiri ukilinganisha na sekta nyingine.
Hayo yameelezwa na wahitimu wa
kidato cha nne 2016 katika Shule ya Mwilamvya Sekondari iliyopo wilayani Kasulu,
wakati wa mahafali ya tisa ya kidato cha nne shuleni hapo.
Aidha wahitimu hao wamesema
kuwa ili mtoto aweze kutimiza ndoto zake yampasa alelewe katika maadili tangu
akiwa mdogo na kwamba kama wazazi nyumbani hawatawalea watoto katika maadili
hawawezi kufanya miujiza wakiwa na walimu shuleni.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Mji wa Kasulu, Scarion Ruhula, ambaye alikuwa mgeni rasmi akimwakilisha Mkuu
wa Wilaya kwenye mahafali hayo amewasihi wazazi na walimu wote kuwa wana jukumu
la malezi ya watoto ili wakaishi vizuri katika jamii hata baada ya kumaliza
masomo yao.
MRADI wa ufugaji wa nyuki ambao upo katika moja ya Miradi
ya Uhifadhi Mazingira Ziwa Victoria (LVEMP II) unakabiliwa na changamoto
mbalimbali zilizosababisha kusuasua kwa mradi huo.
Akizungumza katika ziara maalumu ya kutembelea miradi ya
Lvemp II wilayani Kwimba Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Kwimba, Pendo Malabeja amesema mwamko
wa jamii juu ya utekelezaji wa miradi hiyo wilayani kwake bado ni mdogo.
Malabeja amesema kuna mizinga
62 katika kata ya Kadashi, lakini ni
mizinga 29 tu ndiyo inayofanya kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
John Mongela amemuomba Mkuu wa Wilaya ya Kwimba kuangalia upya miradi ya Lvemp II, kwani inaonekana haiko vizuri.
Aidha amemuagiza pia Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wake
wahakikishe kila ndani ya siku tatu za wiki wanatembelea miradi ya Lvemp II na kuiwekea usimamizi mzuri,
kwani inaonekana fedha nyingi zinaliwa huku miradi hiyo ikisuasua.
Walioshuhudia
wanasema kuwa wapiganaji hao wa Jihad
walichuka eneo hilo muda tu baada ya wanajeshi hao kuondoka.
Mamia
ya watu wameanza kulitoroka eneo hilo wakihofia mashambulio ya kundi hilo.
Hii
ni mara ya tatu mwezi huu ambapo wanajeshi wa Ethiopia wameondoka katika kambi muhimu nchini Somalia.
Imedaiwa
kuwa huenda wanajeshi hao watahitajika kukabiliana na maandamano yanayoendelea
nchini mwao.
Mashambulio
ya angani yameripotiwa katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na yale
yanayokaribiana na maeneo ya Sheikh
Saeed na Salah el-Deen.
Maeneo
mengine yanayoshikiliwa na waasi pia yanalengwa katika mashambulio hayo japo
haijabainika iwapo yanatekelezwa na ndege za Urusi au Syria.
Umoja
wa Mataifa umesema haukufanikiwa kumuondoa mtu yeyote katika maeneo yanayodhibitiwa
na waasi ambayo yamezingirwa wakati wa kipindi cha usitishwaji mapigano kwa
sababu maafisa wake hawakuhakikishiwa usalama wa kuendeleza shughuli hiyo.
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM-Bara, ameelezea
kufurahishwa kwake kufukuzwa kwa wanachama 100 mkoani Mwanza.
======== ========= =========
Imeelezwa kuwa watoto wa kike
wana nafasi kubwa ya kutimiza ndoto zao endapo wataamua kutoyakimbia masomo ya
sayansi.
=========== ==========
Na katika duru za kimataifa,
Post a Comment