0

Mechi pekee ambayo Messi hajafunga kati ya mechi sita zilizopita ni ile ambayo alitolewa nje baada ya kupata majeraha. Na huo ulikuwa ni mchezo mgumu kwa Barcelona dhidi ya Atletico Madrid.
Goli lake la penati dhidi ya Valencia limemfanya kuwa mchezaji pekee aliyefunga magoli mengi dhidi ya Valencia kwenye michezo ya La Liga. Ameifunga Valencia magoli 19 katika mechi za La Liga.
Baada ya kupata majeraha mwezi September, Messi alipata muda wa kupumzika baada ya kupita katika kipindi kigumu kwenye majira ya joto lakini kwa sasa amerejea akiwa na makali yake ya kufumania nyavu.
Wakati Argentina ikiwa inasuasua katika harakati zake za kufuzu kucheza Kombe la Dunia, Messi atahitajika kwenye timu ya taifa wiki chache zijazo. November 11, 2016 Argentina itacheza dhidi ya Brazil kwenye mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia.
Kiwango cha Messi wiki hii kimekuwa ni cha juu. Hat-trick yake iliishuhudia Manchester City iliyo chini ya Pep Guardiola ikilala bao 4-0 ugenini kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Jumamosi, Messi akafunga mara mbili na kufikisha magoli sita katika mechi tatu alizocheza.
Messi anaweza asishinde Ballon d’Or mwaka huu lakini anatengeneza mazingira mazuri ya baadaye kutokana na rekodi za sasa.

Post a Comment

 
Top