MIKUTANO
Wakazi wa kitongoji cha kanyamwanza kata ya mwabaruhi wilayani sengerema wametakiwa
kujitokeza kwenye mikutano ya kijiji
ambayo huitishwa na viongozi kwa ajili ya maendeleo ya maeneo yao.
Hayo
yamesemwa na mwenyekiti wa kitongoji cha kanyamwanza
Bw. INNOSENT SEGEREDI ambapo amesema
wananchi wamekuwa hawajitokezi kwenye mikutano ya kijiji ili kusomewa mapato na
matumizi na kujadili shughuli za maendeleo.
Kwa
upande wao wananchi wa eneo hilo wamekiri kutohudhuria mikutano hiyo hivyo
wamewataka viongozi wa kijiji hicho kuongeza hamasa ya kualika wananchi ikiwa
ni pamoja na kujiwekea sh
TUKIO
Mtu
mmoja ambaye hajafahamika mara moja jina
lake wala makazi yake amekamatwa na
Jeshi la polisi wilayani Sengerema baada
ya kufanya kitendo cha kujizulu mwili kwa kujikata tumbo lake kwa kutumia kisu.
Mtu huyo aliyekamatwa na vyombo vya usalama
ametiwa nguvuni akiwa katika eneo la
kituo cha Habari na mawasiliano Sengerema Telecentre.
Mpaka
sasa haijafahamika chanzo cha kutaka
kufanya kitendo hicho ingawa mashuhuda
wa tukio waliomuona wakati anafika
kituoni hapo wanasema awali wakati
anafika eneo hilo alikuwa anafukuzwa na
wananchi.
Mashuhuda
hao wameeleza kuwa tukio hilo ni la ajabu na la kusikitisha kutokana na kitendo hicho
cha kujikata tumbo lake hali iliyopelekea utumbo kutokeza kwa nje.
Kufuatia
Tukio hilo, Radio Sengerema inaendelea
kuwatafuta viongozi wenye mamlaka ili kupata tamko la serikali kuhusiana
na tukio hilo.
USALAMA
BARABARANI.
Kamanda Mkuu wa
kitengo cha usalama barabarani wilayani sengerema mkoani Mwanza,
Insipecta Hamis Wembo, amewaasa
madereva kuvaa sare zao ili kuwatofautisha kati yao na abiria.
Insipecta Wembo
ameyasema hayo wakati akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu kuwa, madereva
na makondakta wote wa magari madogo na mabasi
makubwa wanatakiwa kuvaa sare ili kuwatenganisha wao na abiria.
Inspekta Wembo ameeleza
kuna mtindo kwa baadhi ya madereva kuvaa sare pindi wanapomuona askari wa
usalama barabarani mbele yao kitu ambacho hakikubariki na wanapaswa kuvaa muda
wote wa safari na wanapaswa kuwa wasafi.
Maelezo
haya yamekuja kufuatia radio sengerema kufanya uchunguzi na kubaini madereva
wanaofanya safari zao sengerema kuelekea Kamanga, na Sengerema kuelekea Buchosa
wengi wao wamekuwa hawana desturi ya kuvaa sare hizo na hivyo kushindwa
kuwatofautisha wawapo kituo cha mabasi.
UPANDAJI MITI
Serikali
kupitia ofisi ya makamu wa rais imesema
kuanzia mwakani kila mwanafunzi anaeanza darasa la kwanza na kidato cha kwanza
atatakiwa kwenda na mti atakaouotesha na kutunza kipindi chote atakapokuwa
shuleni.
Kauli
hiyo imetolewa na waziri wa nchi ofsi ya makamu wa rais muungano na mazingira January Makamba mara baadaya kutembelea
na kushiriki zoezi la upandaji miti katika shule ya msingi Mlandege wilayani Iringa
na kusema kuwa kwa kufanya hivyo nchi itakuwa na miti ya kutosha.
Kwa
upande wake mkuu wa mkoa wa Irinaga
Amina Masenza amesema atasimamia zoezi pamoja na kuwatoa wakulima wanao
lima karibu na vyanzo vya maji huku wanafunzi walioshiriki katika kupanda miti
na waziri Makamba amewahimiza kuitunza
miti hiyo.
TASAF
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Angellah Kairuki amesema jumla ya
kaya 5457 zitaondolewa katika mpango wa kukomboa kaya masikini kutokana na
kutokuwa na sifa za kupata msaada huo.
Akizungumza mbele ya
watendaji na wasimamizi wa halmashauri Kairuki
amesema idadi hiyo imesababisha upotevu wa fedha nyingi ambazo
hazikuwafikia walengwa wa mradi huo.
Ameongeza kuwa kaya hizo
hewa hazitapewa fedha hizo kwa awamu ijayo ya nane na badala yake
kaya stahiki ambazo ni asilimia 76 zitaingia kwenye mpango huo.
Awali akisoma taarifa ya
utekelezaji wa mradi huo Mratibu wa TASAF Esterine
Sephania amesema licha ya kuwepo kwa changamoto kadha wa kadha mradi huo
umesaidia kubadili hali za uchumi wa kaya masikini.
KIMATAIFA
Wagombea wa kiti cha urais
nchini Marekani Hillary Clinton na Donald Trump wamelumbana vikali katika
mdahalo wa tatu na wa mwisho ikiwa zimebaki siku chache kabla ya uchaguzi mkuu
kufanyika.
Wagombea wote wawili
wameelezea masuala mbalimbali ikiwemo uhamiaji, uchumi, majaji wa mahakama kuu,
mizozo ya kimataifa, na haki za wachache.
Mada nyingine zilizogusiwa
ni utoaji mimba, matumizi ya serikali, sheria ya umiliki wa silaha na mengine
mengi.
Mgombea wa chama cha Republican Donald Trump ameonyesha
dalili za kuyakataa matokeo ikiwa atashindwa akisema kura zinaweza kuibiwa.
Kwa mujibu wa Utafiti
uliofanywa na kituo cha televisheni cha CNN, asilimia 52 ya watazamaji wamesema
Clinton kutoka chama cha Democratic ameshinda mdahalo huo huku
asilimia 39 wakisema ni Trump.
KIMATAIFA
Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki-moon ameelezea
matumaini kwamba makubaliano yaliofikiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo ya kuchelewesha uchaguzi hadi mwaka 2018 yatasaidia kuimarisha haki za
binaadamu na kusababisha kuwepo kwa uchaguzi wa kuaminika.
Taarifa iliyotolewa na Umoja
wa Maatifa imesema Ban anazingatia
makubaliano hayo na anatumai kwamba utekelezaji wake utachangia kuweka
mazingira ya kuheshimiwa kwa haki za binaadamu na uhuru ambavyo ni muhimu kwa
mjadala wa kisiasa na uchaguzi unaoaminika.
Katibu Mkuu huyo ameitaka
serikali ya Kongo kuendelea na hatua
za kujenga imani na upinzani, hasa kwa kuwaachia wafungwa wa kisiasa na
kuheshimu haki ya mikusanyiko ya amani.
Maandamano ya kumpinga Rais Joseph Kabila mwezi uliopita yaligeuka
kuwa machafuko na watu wapatao 49 waliuawa.
MICHEZO NA BURUDANI
Ligi kuu Tanzania bara imeendelea tena
leo huku vinara wa ligi kuu Stimu ya simba wakiibuka kidedea kwa
kuwafunga Mbao Fc kwa goli 1-0 katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.
Mtanange huo ulianza kwa kushambuliana kwa
zamu huku simba sport wakionekana kukamia kupata magoli ya mapema, lakini mpka
dakika za lala salama wanafanikiwa kufunga goli hilo.
======= ======= =======
Lionel Messi
alifunga hat-trick dhidi ya Manchester City iliokuwa na safu ya
ulinzi ilio legea huku kipa Claudio
Bravo akipewa kadi nyekundu kwa kushika mpira.
Barcelona inaongoza
kundi C na pointi tisa ,ikiwa mbele kwa pointi tano.
=====
====== ======
Post a Comment