Mchezaji mmoja anayecheza kwenye ligi kuu ya Nigeria, Izu Joseph amepigwa risasi na kufariki nyumbani kwake katika jimbo la Bayelsa kusini mwa nchi hiyo.
Izu Joseph
Mwaandishi wa BBC anasema kuwa Izu alikuwa ni beki wa timu ya Shooting Stars, aliuawa na askari waliokuwa wakikabiliana na wanamgambo katika eneo lenye utajiri wa mafuta.
Miezi ya hivi karibuni kumeshuhudiwa mapigano mapya katika eneo la Delta, huku wapiganaji wakitaka kupewa sehemu ya utajiri wa mafuta.
Post a Comment