0
Usiku wa October 25 2016 michezo 6 ya Kombe la EFL ilichezwa England, moja kati ya mchezo uliochezwa usiku huo ulikuwa ni mchezo kati ya Liverpool dhidi ya Tottenham Hotspurs, mchezo huo ulichezwa katika dimba la Anfield.
Liverpool wakiwa nyumbani walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, magoli ya Liverpool yakifungwa na Daniel Sturridge dakika ya 9 baada ya kutumia vyema assist kutoka kwa Marko Grujic, goli la pili alifunga dakika ya 65 baada ya kupokea assist ya Georginio Wijnaldum, wakati goli la Spurs lilifungwa na Vincent Janssen dakika ya 76 kwa mkwaju wa penati

Post a Comment

 
Top