TAARIFA YA HABARI KUTOKA RADIO SENGEREMA FM
RAIS KUSHIRIKI
IBADA
Rais Dkt. John Pombe
Magufuli, leo ameungana na Waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano lililopo Posta Jijini Dar es
Salaam kusali ibada ya Jumapili ya kuadhimisha Siku ya Bwana ya 19 baada ya
Pentekoste.
Akizungumza na Waumini wa Kanisa hilo baada ya kumalizika kwa
Ibada, Rais Magufuli aliyeongozana
na Mkewe Mama Janeth Magufuli
amewashukuru Viongozi na Waumini wa Kanisa la Anglikana na Madhehebu mengine ya
Dini hapa nchini kwa kuendelea kuliombea Taifa na kudumisha amani na utulivu.
Dkt. Magufuli
amesisitiza kuwa Viongozi wa Dini wanafanya kazi kubwa na muhimu katika Taifa
na kwamba Watanzania wote bila kujali dini zao, itikadi za kisiasa, makundi na
kanda zao wana wajibu wa kuungana na Viongozi hao ili nia hiyo njema iendelee
kufanikiwa.
Kwa upande wake Padre
Jackson Sostenes aliyeongoza Ibada hiyo amemshukuru Rais Magufuli kwa
kuungana na waumini wa Kanisa hilo katika ibada ya Jumapili na ameahidi kuwa Viongozi na
Waumini wa Kanisa hilo wataendelea kumuombea na kuliombea Taifa.
Katika Ibada hiyo Rais Magufuli
ametoa Shilingi Milioni moja kuchangia vikundi vya kwaya vya kanisa hilo.
Na, Mhariri
Twimanye Chanzo Mpekuzi.
VITHIBITI
MWENDO
Wakazi
wa kijiji cha Tabaruka Wilayani
Sengerema wameitaka serikali kuchukua jitihada za
makusudi kuweka vithibiti mwendo
katika barabara itokayo mjini Sengerema hadi Busisi ili
kunusuru vifo vya watoto
vinavyosababishwa na ajali za
barabarani.
Matamshi
ya wakazi hao yanakuja
siku chache baada ya wanafunzi
wawili wa shule ya msingi
Tabaruka kupoteza maisha kwa
kugongwa na gari .
Katika mahojiano
na Radio Sengerema
wananchi wamedai kuwa ukosefu
wa vithibiti mwendo ni chanzo
kinachosababisha ajali za
barabara, na serikali kubaki
kuwatupia lawama wakazi wa eneo hilo
pekee badala ya madereva.
Kwa upande wake
Mkuu wa usalama barabarani
Wilayani Sengerema Inspecta Hamis
Wembo amewaomba wazazi kuwaangalia watoto
pindi wanapovuka barabara ili kuepuka
ajali hizo wakati serikali
ikilitafutia ufumbuzi suala la kuweka
vithibiti mwendo katika barabara hiyo.
Aidha ukosefu
wa vithibiti mwendo katika kijiji cha Tabaruka limekuwa ni tatizo
la muda mrefu bila kupatiwa
ufumbuzi. .
MAFUNZO.
Wananchi
wilayani Sengerema
mkoani Mwanza wametakiwa kujikita
katika mafunzo
ya teknolojia, ufundi pamoja na
ujasiliamali ili waweze kujikwamua kimaisha.
Kauli
hiyo imetolewa na msimamizi wa taasisi
ya Elabs inayojishughulisha na shughuli za kijamii ikiwemo kuwawezesha
vijana Wilayani Sengerema Bi.
Jackline Dismas katika mkutano
wa kuwahamasisha vijana kujiunga na
mafunzo hayo uliofanyika kata ya Sima.
Bi.Jacline, amesema
hatua ya kuitisha mkutano huo imekuja
baada ya wananchi kuoomba yawepo mafunzo
hayo ili waondokane na umasikini.
Aidha
msimamizi wa taasisi hiyo amebainisha kuwa
wameamua kuhamasisha suala hilo kutokana na wananchi wilayani hapa kuwa na mwitikio mkubwa wa kujitokeza
kwenye mafunzo hayo.
Veronica
/Mhariri Twimanye Chanzo
Mkutano .
KUMWENZI BABA WA TAIFA
Katika kuelekea kuadhimisha
kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo
cha Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage
Nyerere Oktoba 14 mwaka huu ,viongozi wa vyama vya Siasa
wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo
aliokuwa nao Baba wa Taifa enzi za uhai
wake, ili kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani mara baada kutembelea Kaburi na Makumbusho ya Baba wa Taifa eneo la Mwitongo wilayani Butiama.
Amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri
katika makumbusho hiyo zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wanasiasa
wanatakiwa kuyafanya kwa vitendo hasa uzalendo kwa nchi, uvumilivu,
upendo na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.
Ameeleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa
na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa
Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa manufaa ya taifa.
Aidha Bw. Kailima amebainisha kuwa NEC itaendelea kumuemzi Baba wa
Taifa kwa yale aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa
wito kwa viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na waridhike na vile
walivyonavyo.
Na,
Mhariri Twimanye chanzo
Mpekuzi.
MAHAFARI.
Shule Msingi
Sayuni iliyopo katika kata Mwabaluhi
Wilayani Sengerema inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa uzio, pamoja na
vifaa vya kufundishia kwa muda
mrefu bila kupatiwa ufumbuzi.
Changamoto hizo
zimebainika katika risala
ya wahitimu iliyosomwa na Shallon
Sinai kwa niaba ya wahitimu wote
mbele ya mgeni rasmi Mchungaji Joakimu
Masama.
Naye
mgeni rasmi Mchungaji Masama akijibu
risala ya wahitimu, amesema kuwa changamoto hizo ataziwasilisha katika kamati
ya shule hiyo ili zitatuliwe.
Kwa
upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Sayuni , Saimon Manoni amesema kuwa shule hiyo
ilianzishwa mwaka 2009 ikiwa na
walimu wawili pekee,
ambapo kwa sasa ina jumla ya walimu 14 wakiwemo
wakike sita na wakiume wanane.
Na,Mhoja/Arafa/Mhariri Twimanye
Chanzo Mahafari.
25/09/2016 KIMATAIFA.
Kiongozi wa
kundi la waasi la Sudan kusini , Riek Machar, ametoa wito wa kuhimiza
vuguvugu la kivita la kuipinga serikali ya nchi hiyo.
Awali bwana Machar alikuwa amerudi katika mji mkuu
wa Juba kama sehemu ya utekelezwaji
wa mkataba wa amani lakini amelazimika kwenda tena uhamishoni Julai mwaka huu, baada ya kuzuka mapigano
yaliyowauwa mamia ya watu .
Taarifa hii
imetolewa baada ya Bwana Machar kukutana na wanachama wa kundi lake huko nchi
jirani ya Sudan.
Hata hivyo
baadhi ya viongozi wa juu wa kundi lake hawamuungi mkono tena.
Mmoja wao ni Taban Deng ambae amejiunga na serikali
amerithishwa wadhifa wa makamu wa rais nafasi iliyokuwa ya Bwana Machar.
Na,
Mhariri Twimanye Chanzo BBC.
KIMATAIFA.
Umoja wa
ulaya umesema mashambulizi yanayoendelea dhidi ya raia katika mji wa Aleppo kaskazini mwa Syria ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za
kimataifa juu ya ubinaadamu, ukitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuzidisha
juhudi za kurejesha amani nchini humo.
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Federica Mogherini, na Kamishina wa
Masuala ya Kibinaadamu, Christos
Stylianides, wamesema mashambulizi dhidi ya raia wasio na hatia ni jambo
lisilokubalika .
Marekani inadai msafara huo ulishambuliwa na
ndege za kivita za Urusi ambayo
inaendesha operesheni ya kijeshi ikiuunga mkono utawala wa Rais Bashar al-Assad.
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema karibu
raia milioni mbili wamekosa huduma ya maji katika mji huo wa kaskazini baada ya
mashambulizi ya mabomu yaliyofanywa na vikosi vya serikali kuharibu mtambo wa
kusukuma maji.
Wakati huo huo, Uingereza, Ufaransa na Marekani
zimetoa wito wa kuitishwa kwa kikao cha haraka cha dharura cha Baraza la
Usalama la Umoja wa Mataifa kujadili juu ya kuendelea kwa mashambulizi katika
mji wa Aleppo.
Na,
Mhariri Twimanye Chanzo DW.
NA
HUO NDIO MWISHO WA TAARIFA YA HABARI
KUTOKA RADIO SENGEREMA FM.
Post a Comment